Zuchu, Nandy Wachuana Kuingiza Mamilioni ya Fedha, noreply@blogger.com (Udaku Special)

September 4, 2020

STORI IBRAHIM YASSIN, Risasi KWENYE ulimwengu wa mastaa wa kike wa Bongo Fleva, warembo; Zuhura Kopa ‘Zuchu’ na Faustina Mfinanga ‘Nandy’ wanachuana vilivyo kuingiza mamilioni ya fedha.Mbali na shoo, Risasi Mchanganyiko limekukusanyia data za mtandao maarufu kwa video za wasanii wa YouTube, ambao unaonesha jinsi gani warembo hao wanaingiza fedha ndefu kutoka kwa wamiliki wa mtandao.Kipimo halisi cha mtandao huo kinaonesha, kwa siku 30 zilizopita, Zuchu amekuja kwa kasi ya ajabu, kwani anaingiza kati ya dola 1900 (shilingi Mil. 4.3) hadi dola 29,000 (shilingi Mil. 66.1), huku Nandy yeye akiingiza kati ya dola 801 (shilingi Mil. 1.8) hadi 12,800 (shilingi Mil. 27.4).Kwa mujibu wa mtandao unaopima kazi hizo, kuna wakati Nandy huwa anapanda juu kumzidi Zuchu, lakini kwa kipindi kirefu, Zuchu ameonekana kumzidi hususan kipindi hiki ambacho mrembo huyo anafatiliwa zaidi baada ya kutoa ngoma mpya kali.Miongoni mwa nyimbo za Zuchu zinazotazamwa zaidi kwa wakati huu, ni pamoja na Raha, Wana, Nisamehe na Hakuna Kulala. Kwa upande wake Nandy, anasumbua na nyimbo zake kali zikiwemo Na Nusu, Kiza Kinene, Acha Lizame na mpya unaokwenda kwa jina la Dozi.Hata kwenye data za jumla, Zuchu anaonekana kuwa juu kwa kuwa anashika nafasi ya 13 wakati Nandy anakamata nafasi 49 kwenye orodha ya wasanii na channel zote za YouTube zilizopo Bongo.Kwenye orodha hiyo, kwa maana ya jumla channel za kibishara na zile binafsi za wasanii, msanii anayeshika nafasi ya juu kwa kutazamwa Bongo, ni Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anayeshika nafasi ya pili, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ ya nane na Rayvanny ya tisa.WANANUFAIKA?Kwa upande wa Nandy, anaweza kuwa ananufaika zaidi na mtonyo huo anaouingiza kila mwezi kwa sababu anafanya kazi akiwa kama bosi, lakini Zuchu yeye yupo chini ya uongozi (Wasafi Classic Baby), hivyo mtonyo ni mpaka upitie kwenye uongozi ndipo urudi kwake.STORI HAPPYNESS MASUNGA, Risasi,

STORI IBRAHIM YASSIN, Risasi KWENYE ulimwengu wa mastaa wa kike wa Bongo Fleva, warembo; Zuhura Kopa ‘Zuchu’ na Faustina Mfinanga ‘Nandy’ wanachuana vilivyo kuingiza mamilioni ya fedha.

Mbali na shoo, Risasi Mchanganyiko limekukusanyia data za mtandao maarufu kwa video za wasanii wa YouTube, ambao unaonesha jinsi gani warembo hao wanaingiza fedha ndefu kutoka kwa wamiliki wa mtandao.

Kipimo halisi cha mtandao huo kinaonesha, kwa siku 30 zilizopita, Zuchu amekuja kwa kasi ya ajabu, kwani anaingiza kati ya dola 1900 (shilingi Mil. 4.3) hadi dola 29,000 (shilingi Mil. 66.1), huku Nandy yeye akiingiza kati ya dola 801 (shilingi Mil. 1.8) hadi 12,800 (shilingi Mil. 27.4).

Kwa mujibu wa mtandao unaopima kazi hizo, kuna wakati Nandy huwa anapanda juu kumzidi Zuchu, lakini kwa kipindi kirefu, Zuchu ameonekana kumzidi hususan kipindi hiki ambacho mrembo huyo anafatiliwa zaidi baada ya kutoa ngoma mpya kali.

Miongoni mwa nyimbo za Zuchu zinazotazamwa zaidi kwa wakati huu, ni pamoja na Raha, Wana, Nisamehe na Hakuna Kulala. Kwa upande wake Nandy, anasumbua na nyimbo zake kali zikiwemo Na Nusu, Kiza Kinene, Acha Lizame na mpya unaokwenda kwa jina la Dozi.

Hata kwenye data za jumla, Zuchu anaonekana kuwa juu kwa kuwa anashika nafasi ya 13 wakati Nandy anakamata nafasi 49 kwenye orodha ya wasanii na channel zote za YouTube zilizopo Bongo.

Kwenye orodha hiyo, kwa maana ya jumla channel za kibishara na zile binafsi za wasanii, msanii anayeshika nafasi ya juu kwa kutazamwa Bongo, ni Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anayeshika nafasi ya pili, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ ya nane na Rayvanny ya tisa.

WANANUFAIKA?

Kwa upande wa Nandy, anaweza kuwa ananufaika zaidi na mtonyo huo anaouingiza kila mwezi kwa sababu anafanya kazi akiwa kama bosi, lakini Zuchu yeye yupo chini ya uongozi (Wasafi Classic Baby), hivyo mtonyo ni mpaka upitie kwenye uongozi ndipo urudi kwake.

STORI HAPPYNESS MASUNGA, Risasi,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *