Zuchu Anabebwa au Jitihada Zake? Jibu Lipo Hapa

September 8, 2020

KATIKA orodha ya wasanii wa kike wanaopepea kwenye gemu la Bongo Fleva, itakuwa ni ngumu kuacha kulitaja jina la Zuchu, msanii chipukizi aliyepokelewa vizuri na mashabiki.Zuchu ni memba mpya wa lebo kubwa inayomilikiwa na mwanamuziki mkubwa hapa Bongo na Afrika Mashariki, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ama Mondi, ya Wasafi Classic Baby (WCB). Jina lake halisi ni Zuhura Othman ambapo mashabiki wanamtambua kama Zuchu.Ni mtoto anayetokea kwenye familia ya vipaji, kwani mama yake mzazi ni mkongwe na malkia wa mipasho hapa Bongo, Bi. Khadija Omari Kopa.Zuchu alisainiwa rasmi miezi mitano iliyopita kama msanii kwenye lebo hiyo na kuongeza idadi ya wasanii wa kike kwenye lebo hiyo, ambapo nafasi ya u-first lady inashikiliwa na mwanamuziki na dada wa Mondi, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’.,

KATIKA orodha ya wasanii wa kike wanaopepea kwenye gemu la Bongo Fleva, itakuwa ni ngumu kuacha kulitaja jina la Zuchu, msanii chipukizi aliyepokelewa vizuri na mashabiki.

Zuchu ni memba mpya wa lebo kubwa inayomilikiwa na mwanamuziki mkubwa hapa Bongo na Afrika Mashariki, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ama Mondi, ya Wasafi Classic Baby (WCB). Jina lake halisi ni Zuhura Othman ambapo mashabiki wanamtambua kama Zuchu.

Ni mtoto anayetokea kwenye familia ya vipaji, kwani mama yake mzazi ni mkongwe na malkia wa mipasho hapa Bongo, Bi. Khadija Omari Kopa.

Zuchu alisainiwa rasmi miezi mitano iliyopita kama msanii kwenye lebo hiyo na kuongeza idadi ya wasanii wa kike kwenye lebo hiyo, ambapo nafasi ya u-first lady inashikiliwa na mwanamuziki na dada wa Mondi, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’.,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *