Zuchu afunguka kuhusu kuwa na bifu na Nandy,

October 17, 2020

 

Msanii mpya wa kizazi kipya, kutoka lebo ya WCB, Zuchu amefunguka kuhusu kuwa na bifu na mwimbaji mwenzie Faustine Mfinaga, Nandy.

Zuchu amesema kuwa yeye na #Nandy hawajawahi kuwa na tatizo na wala hawana tatizo lolote, ila kinachotokea ni watu tu kuwashindanisha.

“Hata Kipindi natoa EP yangu Nandy aliipost, huwezi kuzuia watu kukushindanisha, kwasababu watakushindanisha tu, lakini nachukia maneno ya watu wanaosema natengenezwa kumshusha Nandy,” amesema Zuchu kwenye mahojiano na WasafiFm Ijumaa hii.

Pia Zuchu ameongelea maneno yanayodai kuwa anatengenezwa ili kumshusha msanii mwenzake Nandy, na kusema maneno hayo yanaongelewa na watu wasio na mapenzi mema kwake ili tu kumtengenezea maadui ambao yeye hawaitaji.

“Nandy ni msanii mzuri na anafanya mambo yake, na mimi natafuta ridhiki yangu ” amesema Zuchu.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *