Zitto Kabwe: Rais Magufuli ampigia simu na kumpa pole kiongozi wa ACT Wazalendo

October 7, 2020

Saa 2 zilizopita

Zitto Zuberi Kabwe

Kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT-wazalendo, Zitto Kabwe aliyehusika katika ajali ya barabarani siku ya Jumanne akiwa na wenzake wanne amesema anaendelea kupata nafuu.

Kupitia ujumbe alioandika kwenye mtandao wake wa Twitter Bw. Zitto alisema: ”Ninaendelea vizuri. Ilikuwa ajali mbaya sana. Namshukuru Allah kwa kutuponya. Shukran Wahudumu wa Kituo cha Afya Kalya, licha ya changamoto, Huduma ya kwanza imetusaidia. Shukran Madaktari na Wahudumu Hospitali ya Maweni Kigoma. Mimi na wenzangu, mpaka sasa, ni wazima.”

Kiongozi huyo na wenzake wanne walipata ajali, jimboni Kigoma Kusini, Magharibi mwa Tanzania.

Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho upande wa bara, Joran Bashange, ajali hiyo ilitokea akiwa kwenye shughuli za kampeni, akitoka katika eneo la kata ya Kalya kuelekea Lukoma.

”Gari lake liligongwa nyuma kisha likapoteza mwelekeo na kupinduka zaidi ya mara mbili.”

Imeelezwa kuwa gari lake lilikuwa na abiria watano ambao wote wako salama, lakini wamepata maumivu na majeraha.

”Wamekwishapata huduma ya kwanza, na chama kimechukua hatua za kukodisha ndege kutoka Kigoma kwenda Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

Akizungumza na BBC,siku ya Jumanne Afisa habari wa chama hicho Arodia Peter amesema bado chama hakijapata taarifa rasmi kama Zitto ameshawasili Dar es Salaam.

Tayari rais John Pombe Magufuli amepigia simu na kumpa pole Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe kwa mujibu wa ujumbe uliochapishwa na mkurugenzi wa mawasiliano ya rais Gerson Msigwa.

Kulingana na Msigwa Magufuli amemuombea heri ili apone haraka na pia akawashukuru madaktari na wauguzi wa kituo cha afya cha kalya na hopsitali ya mawezini kwamatibabu waliompa.

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *