Zitto amvaa Kitila “anatumia ilani ya ACT”, on September 6, 2020 at 5:00 pm

September 6, 2020

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe amesema kuwa ilani ya Chama chao imekuwa ikitumiwa na vyama vingine kwa kile alichodai imeandikwa kwa ustadi na kufanyiwa utafiti.Zitto ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa baadhi ya wagombea wa Chama cha Mapinduzi wanatumia ilani yao katika kujinadi.Aidha amesema kuwa wabunge wao zaidi ya hamsini wameenguliwa Nchi nzima, hivyo wana subiria majibu ya mapingamizi waliyotuma Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).“Ilani ya ACT Wazalendo inasemekana ndio bora kuliko zote, hata CCM wanatumia ilani yetu akiwemo Profesa Kitila Mkumbo mgombea Ubunge CCM Jimbo la Ubungo ambaye ameahidi kujenga Arena Wilaya ya Ubungo kitu ambacho ilani ya chama chake haina hilo wazo”, amesema Zitto.Zitto pia ameongeza kuwa hana imani kama ni kweli wagombea wa upinzani pekee ndio wamekosea kujaza fomu za uteuzi wa kugombea nafasi za Ubunge na Udiwani.,

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe amesema kuwa ilani ya Chama chao imekuwa ikitumiwa na vyama vingine kwa kile alichodai imeandikwa kwa ustadi na kufanyiwa utafiti.

Zitto ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa baadhi ya wagombea wa Chama cha Mapinduzi wanatumia ilani yao katika kujinadi.

Aidha amesema kuwa wabunge wao zaidi ya hamsini wameenguliwa Nchi nzima, hivyo wana subiria majibu ya mapingamizi waliyotuma Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

“Ilani ya ACT Wazalendo inasemekana ndio bora kuliko zote, hata CCM wanatumia ilani yetu akiwemo Profesa Kitila Mkumbo mgombea Ubunge CCM Jimbo la Ubungo ambaye ameahidi kujenga Arena Wilaya ya Ubungo kitu ambacho ilani ya chama chake haina hilo wazo”, amesema Zitto.

Zitto pia ameongeza kuwa hana imani kama ni kweli wagombea wa upinzani pekee ndio wamekosea kujaza fomu za uteuzi wa kugombea nafasi za Ubunge na Udiwani.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *