Zimbabwe kuwafidia wazungu waliopokonywa mashamba yao, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on September 1, 2020 at 1:00 pm

September 1, 2020

Wakulima wazungu 3,500 walifurushwa kutoka kwa mashamba yao karibu miaka 20 iliyopitaImage caption: Wakulima wazungu 3,500 walifurushwa kutoka kwa mashamba yao karibu miaka 20 iliyopitaSerikali ya Zimbabwe imesema kwamba wakulima wazungu ambao walipokonywa ardhi zao kati ya mwaka 2000 na 2001 wanaweza kutoa maombi ya kurudishiwa ardhi hizo chini ya mpango mpya wa mageuzi ya sera ya ardhi.Ikiwa ardhi haitaweza kurudishwa, wakulima hao watapewa ardhi sehemu nyingine, kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa na Mawaziri wa Fedha Mthuli Ncube na wa Ardhi Anxious Masuka.Mawaziri hao wamesema watafutilia mbali barua zilizowapa idhini wakulima weusi kuchukua ardhi hizo.Walisema wakilima wazungu ambao ardhi zao zilichukuliwa na serikali na ambazo hazijatolewa wanaweza kutoa maombi ya kuzikodisha kwa miaka 99.Wakulima wazungu 3,500 walifurushwa kutoka kwa mashamba yao wakati wa marekebisho tata ya sera ya ardhi.Serikali ya Zimbabwe mwezi Mei ilikubali kuwafidia dola bilioni 3.5 wakulima wazungu ambao ardhi zao zilichukuliwa enzi za utawala wa rais wa zamani wa nchi hiyo marehemu Robert Mugabe.,

Wakulima wazungu 3,500 walifurushwa kutoka kwa mashamba yao karibu miaka 20 iliyopitaImage caption: Wakulima wazungu 3,500 walifurushwa kutoka kwa mashamba yao karibu miaka 20 iliyopita

Serikali ya Zimbabwe imesema kwamba wakulima wazungu ambao walipokonywa ardhi zao kati ya mwaka 2000 na 2001 wanaweza kutoa maombi ya kurudishiwa ardhi hizo chini ya mpango mpya wa mageuzi ya sera ya ardhi.

Ikiwa ardhi haitaweza kurudishwa, wakulima hao watapewa ardhi sehemu nyingine, kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa na Mawaziri wa Fedha Mthuli Ncube na wa Ardhi Anxious Masuka.

Mawaziri hao wamesema watafutilia mbali barua zilizowapa idhini wakulima weusi kuchukua ardhi hizo.

Walisema wakilima wazungu ambao ardhi zao zilichukuliwa na serikali na ambazo hazijatolewa wanaweza kutoa maombi ya kuzikodisha kwa miaka 99.

Wakulima wazungu 3,500 walifurushwa kutoka kwa mashamba yao wakati wa marekebisho tata ya sera ya ardhi.

Serikali ya Zimbabwe mwezi Mei ilikubali kuwafidia dola bilioni 3.5 wakulima wazungu ambao ardhi zao zilichukuliwa enzi za utawala wa rais wa zamani wa nchi hiyo marehemu Robert Mugabe.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *