ZEC yawaonya waangalizi kuelekea Uchaguzi Mkuu Zanzibar

October 1, 2020

Baada ya mchujo mkali wa jumuiya zisizo za kiserikali zilizoomba kushiriki utoaji wa elimu na uangalizi wa uchaguzi hatimae tume ya uchaguzi imetoa vibali kwa taasisi 15 zikiwemo za jumuiya za kanda za Afrika Mashariki na Ulaya.

Akizungumzia kuhusu muongozi huo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jaji Mkuu Mstaafu Hamid Mahmoud amewaambia waliopewa kibali wahakikishe wanafuata sheria na muongozo waliopewa kama walivyaoaminiwa.

Taasisi zilizopewa vibali kufuata muongozo uliotolewa

Miongoni mwa waliopata vibali vya utoaji wa elimu na uangalizini asasi za kiraia zikiwemo zile za vijana, wanawake na makundi maalumu wakiwemo watu wenye ulamavu. Mratibu wa Jumuiya Watu wenye ulamavu Zanzibar Donard Naveta anaelezea.

Sansibar | Präsidentschaftskandidat Hussein Mwinyi legt Wahlkomission Formale vor (DW/S. Said)

Hussein Mwinyi mgombea wa urais zanzibar kupitia CCM

Taasisi ambazo zimepatiwa vibali zimepewa masharti maalumu ya kufanya kazi ikiwemo kufuata muongozo waliopewa, kutoa ratiba ya mikutano yao ya utoaji elimu kwa wale ambao wamepewa kibali tu bila ya kushirikiana na taasisi nyengine ambayo haikupewa kibali.

Salma Saadat ni mmoja wa watoaji wa elimu ambaye taasisi yake inayowakilisha wanawake imepatiwa kibali anaeleza namna walivyopewa muongozo na tume.

Taasisi nyingi za utoaji elimu zimenyimwa vibali

Mkurugenzi wa Uchaguzi Thabit Idarous Faina amesema matayarisho yote yamekamilika kama yalivyopangwa.

Taasisi nyingi ambazo zimeomba kibali cha utoaji wa elimu na uangalizi wa uchaguzi zimenyimwa kibali. Huyu hapa ni mmoja wa waliokosa kibali.

Kwa mujibu wa sheria mpya ya uchaguzi taasisi za kidini zimetolewa kwenye uangalizi tofauti na chaguzi zilizopita.

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *