Zaidi ya wanajeshi 2,200 wa Marekani kuondoka Iraq mwezi huu

September 9, 2020

Dakika 4 zilizopita

File photo showing US soldiers during a handover ceremony of Taji military base to Iraqi security forces (23 August 2020)

Maelezo ya picha,

Wanajeshi wa Marekani wamekuepo Iraq tangu mwaka 2014 kupambana na IS

Marekani itaondoa zaidi ya robo tatu ya jeshi lake nchini Iraq ndani ya wiki kadhaa, kamanda mkuu wa Mashariki ya kati amesema.

Gen Kenneth McKenzie amewaambia waandishi wa habari kuwa jeshi litapunguzwa kutoka wanajeshi wapatao 5,200 mpaka 3,000 ndani ya mwezi huu wa Septemba.

Hao watakaosalia wataendelea kuwashauri na kusaidia vikosi vya usalama vya Iraq kukabiliana na kundi la wapiganaji wa kiislamu la ‘Islamic State (IS)’.

Mwezi uliopita, rais Donald Trump alisema kuwa Marekani ina mpango wa kuondoa jeshi lake Iraq mapema iwezekanavyo.

Trump anatarajiwa kuchukua hatua hiyo baada ya kutoa ahadi katika kampeni iliyopita kuwa anataka kuiondoa Marekani katika kile anachokielezea kuwa vita isiyoisha.

Uwepo wa jeshi la Marekani limekuwa tatizo kubwa Iraq tangu Marekani ilipohusika kumuua kiongozi wa ngazi ya juu nchini Iran Qasem Soleimani katika mapigano ya anga mjini Baghdad mwezi Januari.

Source link

,Dakika 4 zilizopita Chanzo cha picha, Reuters Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Marekani wamekuepo Iraq tangu mwaka 2014 kupambana na…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *