Zaidi ya raia 500 wauawa nchini Afghanistan tangu mwanzo wa mwaka,

October 4, 2020

Tume huru ya haki za binadamu nchini Afghanistan imesema takriban raia 533 waliuawa nchini humo katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo, watu wengine 945 walijeruhiwa katika kile shirika hilo lilitaja kuwa ”mauaji ya kupangwa.

”Shirika hilo limesema kuwa kati ya mwezi Februari na Septemba, raia 122 waliuawa na wengine 72 walijeruhiwa katika mashambulizi dhidi ya eneo la Kusini la Kandahar.Ripoti hiyo inajiri siku moja baada ya bomu lililotegwa katika gari kulipuka na kuwauwa watu 14 na kuwajeruhi wengine 42 wengi wao wakiwa raia katika eneo la Mashariki mwa mkoa wa Nangahar. 

Hakuna kundi lililodai kuhusika katika mashambulizi hayo lakini serikali ya Afghanistan imelilaumu kundi la Taliban kwa tukio hilo. 

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *