Yoshihide Suga achaguliwa Waziri mkuu wa mpya wa Japan baada ya Shinzo Abe

September 16, 2020

Dakika 3 zilizopita

Yoshihide Suga

Maelezo ya picha,

Yoshihide Suga, waziri mkuu mpya wa Japan

Bunge la Japan limemchagua Yoshihide Suga kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo, kufuatia hatua ya Shinzo Abe kujiuzulu.

Baada ya kushinda uongozi wa chama tawala mapema wiki hii, kura ya Jumatano imeidhinisha rasmi wadhifa wa mkuu huyo zamani wa mawaziri.

Waziri mkuu huyo mpya ambaye ni mshirika wa karibu wa bwana Abe, anatarajiwa kuendeleza sera ya mtangulizi wake.

Shinzo Abe alitangazi kujiuzulu kwake mwezi uliopita kutokana na sababu za afya.

Mapema Jumatano, Bw. Abe alifanya mkutano wake wa mwisho wa mawaziri na kuwaambia wanahabari kwamba anajivunia utawala wake wa karibu miaka minane.

Bwana Suga alishinda kirahisi katika uchaguzi wa waziri mkuu katika bunge la Diet, ambalo ni la chini nchini Japan, baada ya kupata 314 kati ya kura zote 462 zilizopigwa

Ikizingatiwa kwamba muungano unaoongozwa na chama chake cha kihafidhina, Liberal Democratic Party (LDP) kina wabunge wengi, ushindi wake ulitarajiwa na wengi.

Yeye pamoja na mawaziri wake wapya baadaye wataidhinishwa rasmi katika hafla itakayoandaliwa katika Imperial Palace.

Changamoto zinazomsubiri

Mwanasiasa huyo mkongwe aliye hudumu serikalini kwa muda mrefu anachukua uongozi katika kipindi kigumu kwa nchi hiyo ambayo uchumi wake ni wa tatu kwa ukubwa duniani

Sawana nchi zingine, Japan inakabiliwa na changamoto ya janga la corona ambayo imeathiri pakubwa uchumi wake ambao umedumaa kwa miaka kadhaa..

Nchi hiyo pia inakabiliwa na ongezeko la wazee katika jamii, ikisadikiwa kuwa karibu thuluthi moja ya raia wake ni wazee walio na miaka zaidi ya 65.

Bwana Suga amehudumu kwa miaka kadhaa kama mkuuu wa mawaziri, wadhifa ambao ni wa pili kwa ukubwa serikalini baada ya waziri mkuu.

Yoshihide Suga

Maelezo ya picha,

Yoshihide Suga baada ya ushindi wake wa Jumatano

Tayari ameahidi kuendeleza ajenda ya utawala uliokuwepo, ikiwa ni pamoja na mpango wa mageuzi wa kiuchumi unaofahamika kama Abenomics.

“Uchaguzi wa Bw. Suga unahakikishia kuendelea kwa mipango yote mikubwa ya sera iliyozinduliwa na Shinzo ,” Yuki Tatsumi, mkurugenzi wa kituo cha Stimson ambacho kinaendesha mipango ya Japan mjini Washington, aliiambia BBC.

“Kitakachokuwa kibarua kikubwa kwake ni ni jinsi atakavyoimarisha mtazamo wa umma dhidi ya serikali ya Japan,” alionya.

Mwana huyo wa mkulima na mwanasiasa mkongwe anatokea katika familia ambayo ya maisha yake yalikuwa ya kawaida sawa na ya Wajapan wengine, hali ambayo inamtofautisha na wanasiasa wengine nchini humo.

Akiwa na umri wa miaka 71- alipanda polepole katika ngazi ya kisiasa nchini humo. Kwanza alifanya kazi kama katibu wa mbunge wa mbunge chama LDP kabla ya kuanza safari yake mwenyewe ya kisiasa, kutoka kwa uchaguzi wa baraza la manispaa hadi kuwa mwanachama wa bunge la Diet mwaka 1996.

2005 aliteuliwa kuwa waziri chini ya Junichiro Koizumi na kupata ushawishi zaidi katika baraza la mawaziri la Bw. Abe.

Kama mshirika wa karibu wa Abe, alijizolea sifa kutokana na utendakazi wake na waziri mkuu anayeondoka aliunga mkono ombi lake la kuwa kiongozi wa nchi.

Source link

,Dakika 3 zilizopita Chanzo cha picha, Reuters Maelezo ya picha, Yoshihide Suga, waziri mkuu mpya wa Japan Bunge la Japan…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *