Yanga Yachekelea, Simba Yashikwa na Kigugumizi

October 8, 2020

KUFUATIA Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kuupeleka mbele mchezo wa Dabi ya Kariakoo unaozikutanisha Simba na Yanga, viongozi wa klabu hizo wameibuka na kuzungumzia ishu hiyo.

Mapema jana Jumatano asubuhi, TPLB ilitoa taarifa ya kufanya mabadiliko ya ratiba ya mchezo huo namba 61 wa ligi kati ya Yanga na Simba kwa sababu ya uwezekano mkubwa wa kuwepo kwa vikwazo katika usafiri wa kimataifa baada ya kukamilika kwa michezo ya kimataifa iliyo kwenye Kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

 

Awali mchezo huo ulipangwa kuchezwa Oktoba 18, mwaka huu, lakini umesogezwa mbele hadi Novemba 7, mwaka huu.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, alisema taarifa hizo wamezipokea vizuri na wao kama klabu hawana pingamizi lolote.

“Kama klabu tumezipokea taarifa hizo na hivi karibuni tutakuwa na kikao cha viongozi ambacho kitatoka na taarifa rasmi lakini licha ya changamoto zake naamini ni maamuzi yanayoangalia maslahi mapana ya pande zote mbili,” alisema Bumbuli.

 

Kwa upande wa Simba, meneja wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu, alisema: “Tumeipokea taarifa hiyo na nisingependa kuzungumza sana, uongozi wa klabu chini ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez utakaa na kutoa taarifa rasmi pamoja na mipango mingine kwa kuwa timu ilishaweka utaratibu wa kuanza mazoezi.”

 

Wakati huohuo, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo, alitolea ufafanuzi zaidi akisema:

“Kumekuwa na taarifa zisizo rasmi kuwa mchezo wa kwanza kati ya Taifa Stars na Tunisia umepangwa kufanyika Novemba 9, mwaka huu kiasi cha kuleta mkanganyiko kwa wadau wa soka.

 

“Taarifa hizo si za ukweli kwani michezo dhidi ya Tunisia ilipangwa kufanyika kati ya Novemba 9 hadi 17 na taarifa rasmi juu ya mchezo wa raundi ya kwanza utakaopigwa kule Tunisia utafanyika Novemba 13, mwaka huu, kisha marudiano ni Novemba 17.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *