Yanga Yabakiza Wachezaji Watano Dar es Salaam

September 18, 2020

YANGA jana iliondoka jijini Dar es Salaam na kikosi cha wachezaji 20 huku ikiwaacha watano.Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wake wa tatu wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera.Yanga itaingia uwanjani ikiwa na wachezaji wote muhimu na tegemeo katika kikosi hicho kilichosajiliwa katika msimu huu ambao wamepania kuuchukua ubingwa wa ligi.Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, na kuthibitishwa na Meneja Mkuu wa timu hiyo, Hafidh Saleh kikosi hicho kimefika salama Bukoba tayari kwa ajili ya mchezo huo kikiwa na wachezaji wote muhimu na tegemeoWachezaji walioachwa Dar ni Wazir Junior ambaye alifunga bao moja walipocheza na Mlandege kwenye mchezo wa kirafiki na kupata ushindi wa mabao 2-0 juzi, Paul Godfrey ‘Boxer’, Juma Mahadhi, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na Farouk Shikalo ambaye anadaiwa kuwa na majeraha.Timu hiyo mara baada ya kutua Bukoba saa 3:45 asubuhi, haraka iliingia kambini tayari kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mchezo ambapo jana jioni ilifanya mazoezi ya pamoja.,

YANGA jana iliondoka jijini Dar es Salaam na kikosi cha wachezaji 20 huku ikiwaacha watano.Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wake wa tatu wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera.

Yanga itaingia uwanjani ikiwa na wachezaji wote muhimu na tegemeo katika kikosi hicho kilichosajiliwa katika msimu huu ambao wamepania kuuchukua ubingwa wa ligi.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, na kuthibitishwa na Meneja Mkuu wa timu hiyo, Hafidh Saleh kikosi hicho kimefika salama Bukoba tayari kwa ajili ya mchezo huo kikiwa na wachezaji wote muhimu na tegemeo

Wachezaji walioachwa Dar ni Wazir Junior ambaye alifunga bao moja walipocheza na Mlandege kwenye mchezo wa kirafiki na kupata ushindi wa mabao 2-0 juzi, Paul Godfrey ‘Boxer’, Juma Mahadhi, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na Farouk Shikalo ambaye anadaiwa kuwa na majeraha.

Timu hiyo mara baada ya kutua Bukoba saa 3:45 asubuhi, haraka iliingia kambini tayari kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mchezo ambapo jana jioni ilifanya mazoezi ya pamoja.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *