Yanga Kutesti Silaha Zake leo Chamazi

October 9, 2020

IKIJIANDAA na mchezo wake dhidi ya Simba pamoja na mingine ijayo, Yanga, leo Ijumaa inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mwadui FC ambao ni wapinzani wao katika Ligi Kuu Bara.

Yanga ambayo ipo kambini Avic Town, Kigamboni, Kimbiji nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, hivi sasa ipo kwenye maandalizi ya nguvu huku ikisubiri kocha mkuu mpya atue klabuni hapo.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Meneja Mkuu wa Yanga, Hafidhi Saleh alisema kuwa mchezo wao na Mwadui FC unatarajiwa kupigwa saa 1:00 Usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar.Saleh alisema mchezo huo maalum ameuomba Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Juma Mwambusi kwa ajili ya kujiandaa na michezo inayofuatia ya ligi

“Timu ipo kambini na kesho (leo) tunatarajia kucheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya Mwadui kwenye Uwanja wa Azam Complex,” alithibitisha Saleh.Nahodha Mkuu wa Mwadui FC, Joram Mgeveke alithibitisha hilo kwa kusema: “Ni kweli tunacheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya Yanga katika kujiandaa na ligi.

“Tulipoteza mechi zilizopita kwa sababu timu ilikuwa na wachezaji wengi wapya ambao tulikuwa hatukuzoeana, hivyo tunatumia mchezo huu dhidi ya Yanga kwa ajili ya kutengeneza muunganiko wa timu.”

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *