Wizara ya mifugo na uvuvi yazitaka taasisi kutumia mfumo wa ulipaji serikalini, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on September 4, 2020 at 10:00 am

September 4, 2020

Wizara ya Mifugo na Uvuvi  imezitaka taasisi zilizo chini ya Sekta ya Mifugo kuhakikisha zinatumia mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE).Agizo hilo limetolewa na katibu Mkuu wa wizara ya mifugo na uvuvi, ,Profesa Elisante Ole Gabriel alipozungumza na washiriki wa mafunzo ya mfumo wa ulipaji serikalini, ambayo yalifanyika jana katika ukumbi wa ofisi ya taifa ya ukaguzi iliyopo jijini Dodoma.Prof. Gabriel amezitaka taasisi hizo zihakikishe zinautumia mfumo huo kwa kuwa utasaidia kuongeza makusanyo ya mapato, utarahisisha ulipaji wa fedha pamoja na kutunza kumbukumbu za matumizi ya fedha.“Kwa kutumia mifumo ya TEHAMA sisi Wizara ya Mifugo kupitia minada tu tumeweza kuongoza ukusanyaji wa mapato mfano mmoja ya mnada uliopo kanda ya Ziwa tulikuwa tukikusanya sh. 720,000 kwa siku lakini baada ya matumizi ya mifumo ya TEHAMA tunakusanya 7,500,000 kwa siku,” alisema Prof. Gabriel.Profesa Gabriel pia aliwasisitiza washiriki kuhakikisha fedha zote zinazokusanywa zinaingizwa kwenye mfumo kabla ya kutumika kwani kwa kutofanya hivyo watakuwa wamekiuka taratibu.Licha ya kutoa agizo hilo, katibu mkuu huyo wa wizara ya mifugo na uvuvi ameipongeza wizara ya fedha na mipango kwa kuendelea kuwatumia wataalamu wa ndani kubuni mifumo mbalimbali ya ukusanyaji mapato pamoja na udhibiti wa matumizi ya mapato hayo.Naye Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA, Tazari Kibola alisema mafunzo hayo yatawawezesha washiriki kujua namna ya kutumia mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE) ambao utasaidia kuongeza ukusanyaji wa mapato na udhibiti wake katika taasisi zao.Alisema baada ya mafunzo hayo watakwenda katika taasisi hizo kuona kama kuna mapungufu ya mahitaji yanayohitajika ili mfumo huo uanze kutumika.Akimshukuru katibu mkuu kwaniaba ya washiriki hao, mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dennis Ndabiriwe alisema kupitia mafunzo hayo na mfumo utakapoanza kutumika utawasaidia kuongeza mapato, hivyo watakwenda kuainisha mahitaji ya mfumo na kuhakikisha wanaanza kuutumia.Mafunzo hayo yamewahusisha Wahasibu, Meneja wa Fedha, watalamu wa manunuzi, maofisa TEHAMA na maofisa bajeti kutoka taasisi za wakala ya vyuo vya mafunzo ya mifugo Tanzania (LITA), Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Bodi ya Nyama, na Bodi ya Maziwa.,

Wizara ya Mifugo na Uvuvi  imezitaka taasisi zilizo chini ya Sekta ya Mifugo kuhakikisha zinatumia mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE).

Agizo hilo limetolewa na katibu Mkuu wa wizara ya mifugo na uvuvi, ,Profesa Elisante Ole Gabriel alipozungumza na washiriki wa mafunzo ya mfumo wa ulipaji serikalini, ambayo yalifanyika jana katika ukumbi wa ofisi ya taifa ya ukaguzi iliyopo jijini Dodoma.

Prof. Gabriel amezitaka taasisi hizo zihakikishe zinautumia mfumo huo kwa kuwa utasaidia kuongeza makusanyo ya mapato, utarahisisha ulipaji wa fedha pamoja na kutunza kumbukumbu za matumizi ya fedha.

“Kwa kutumia mifumo ya TEHAMA sisi Wizara ya Mifugo kupitia minada tu tumeweza kuongoza ukusanyaji wa mapato mfano mmoja ya mnada uliopo kanda ya Ziwa tulikuwa tukikusanya sh. 720,000 kwa siku lakini baada ya matumizi ya mifumo ya TEHAMA tunakusanya 7,500,000 kwa siku,” alisema Prof. Gabriel.

Profesa Gabriel pia aliwasisitiza washiriki kuhakikisha fedha zote zinazokusanywa zinaingizwa kwenye mfumo kabla ya kutumika kwani kwa kutofanya hivyo watakuwa wamekiuka taratibu.

Licha ya kutoa agizo hilo, katibu mkuu huyo wa wizara ya mifugo na uvuvi ameipongeza wizara ya fedha na mipango kwa kuendelea kuwatumia wataalamu wa ndani kubuni mifumo mbalimbali ya ukusanyaji mapato pamoja na udhibiti wa matumizi ya mapato hayo.

Naye Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA, Tazari Kibola alisema mafunzo hayo yatawawezesha washiriki kujua namna ya kutumia mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE) ambao utasaidia kuongeza ukusanyaji wa mapato na udhibiti wake katika taasisi zao.

Alisema baada ya mafunzo hayo watakwenda katika taasisi hizo kuona kama kuna mapungufu ya mahitaji yanayohitajika ili mfumo huo uanze kutumika.

Akimshukuru katibu mkuu kwaniaba ya washiriki hao, mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dennis Ndabiriwe alisema kupitia mafunzo hayo na mfumo utakapoanza kutumika utawasaidia kuongeza mapato, hivyo watakwenda kuainisha mahitaji ya mfumo na kuhakikisha wanaanza kuutumia.

Mafunzo hayo yamewahusisha Wahasibu, Meneja wa Fedha, watalamu wa manunuzi, maofisa TEHAMA na maofisa bajeti kutoka taasisi za wakala ya vyuo vya mafunzo ya mifugo Tanzania (LITA), Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Bodi ya Nyama, na Bodi ya Maziwa.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *