Wizara ya Afya Kenya yaagizwa kuchapisha zabuni za Covid-19, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on September 1, 2020 at 10:00 am

September 1, 2020

 Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameamuru wizara ya afya kuchapisha zabuni zote zinazohusiana na jinsi serikali ilivyoshughulikia janga la Covid-19.Zabuni zinazotakiwa kuchapishwa ni zile zilizotolewa na mamlaka ya usambazaji vifaa vya matibabu nchini Kenya(Kemsa).Amri ya rais inafuatia madai ya ubadhirifu wa fedha za umma uliokumba machakato wa kutolewa kwa zabuni hizo.Wabunge wameanza uchunguzi binafsi kuhusiana na madai hayo.Afisa mkuu mtendaji wa Kemsa wiki iliyopita alifahamisha kamati ya bunge la seneti kwamba alipokea maelekezo kutoka waziri wa afya Mutahi Kagwe na katibu mkuu katika wizara hiyo Susan Mochache kuhusu jinsi ya kutoa zabuni hizo.Wawili hao wamesema hawajafanya kosa lolote.”Wizara ya Afya, katika kipindi cha siku 30 zijazo, lazima libuni njia mwafaka na iliyo wazi itakayoonesha jinsi Kemsa ilivyotangaza na kupeana zabuni hizo,” Rais Kenyatta alisema hayo siku ya Jumatatu wakati alipoongozo kongamano la magavana kuhusu Covid-19.,

 

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameamuru wizara ya afya kuchapisha zabuni zote zinazohusiana na jinsi serikali ilivyoshughulikia janga la Covid-19.

Zabuni zinazotakiwa kuchapishwa ni zile zilizotolewa na mamlaka ya usambazaji vifaa vya matibabu nchini Kenya(Kemsa).

Amri ya rais inafuatia madai ya ubadhirifu wa fedha za umma uliokumba machakato wa kutolewa kwa zabuni hizo.

Wabunge wameanza uchunguzi binafsi kuhusiana na madai hayo.

Afisa mkuu mtendaji wa Kemsa wiki iliyopita alifahamisha kamati ya bunge la seneti kwamba alipokea maelekezo kutoka waziri wa afya Mutahi Kagwe na katibu mkuu katika wizara hiyo Susan Mochache kuhusu jinsi ya kutoa zabuni hizo.

Wawili hao wamesema hawajafanya kosa lolote.

“Wizara ya Afya, katika kipindi cha siku 30 zijazo, lazima libuni njia mwafaka na iliyo wazi itakayoonesha jinsi Kemsa ilivyotangaza na kupeana zabuni hizo,” Rais Kenyatta alisema hayo siku ya Jumatatu wakati alipoongozo kongamano la magavana kuhusu Covid-19.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *