Will Smith amwaga machozi baada ya mkewe kuchepuka

October 7, 2020

 

Hiyo picha ime-trend sana mitandaoni mwezi Julai ikimuonyesha mchekeshaji na muigizaji Will Smith (52) kama analia, kutia huruma na kuwa mnyonge baada ya mkewe Jada Pinkett Smith (49) kumwambia ukweli kwamba alichepuka na msanii August Alsina (28).

 

Sasa mchekeshaji huyo amefunguka kuhusu picha hiyo wakati anataniana na mkewe Jada Pinkett kwa kusema “Nilikunywa sana kahawa usiku ule na nilikuwa ‘high’ na macho yangu yalihitaji maji, watu walifikiri kama nilikuwa nalia muda wote lakini sio kweli nilikuwa silii, halafu tulirekodi usiku wa manane kwa sababu tulikuwa tunawahi ‘Airport’ asubuhi yake, na nilikuwa nimechoka”.

Picha hiyo ikimuonesha Will Smith kama analia na kutia huruma ilitumika kama moja wapo ya vitu vya kuchekesha yaani ‘Memes’ kwenye mitandao ya kijamii.

Wiki iliyopita mtoto wao wa kike Willow Smith alimpongeza mama yake Jada Pinkett kwa ujasiri wa kumwambia ukweli baba yake mbele ya TV show yao ya ‘Red Table Talk’ kama alichepuka na mwanaume mwingine.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *