WFP yaonya kuwa mamilioni ya watu wanakabiliwa na baa la njaa, on September 18, 2020 at 3:00 pm

September 18, 2020

 Mkuu wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP, ameonya kuwa mamilioni ya watu wanakabiliwa na baa la njaa kutokana na mizozo, mabadiliko ya tabia nchi na janga la Covid-19.David Beasley ametoa wito kwa wahisani kusaidia kukabiliana na hali hiyo.Mkuu huyo wa shirika la mpango wa chakula duniani ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa kufanyiwa kazi onyo alilolitoa miezi mitano iliyopita kumesaidia kuzuia janga la njaa.Beasley amesema shirika la WFP na washirika wake wamejaribu kuwafikia watu milioni 138 mwaka huu, idadi hiyo ikiwa kiwango kikubwa cha watu kusaidiwa katika historia na shirika hilo.Hata hivyo ameonya kuwa watu milioni 270 wanakabiliwa na njaa. Tayari watu milioni 30 wanategemea chakula kutoka WFP na huenda wakafariki iwapo watakosa msaada huo.Mataifa ambayo watu wake wanakabaliwa na njaa ni Congo, Yemen, Sudan Kusini na Nigeria.,

 

Mkuu wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP, ameonya kuwa mamilioni ya watu wanakabiliwa na baa la njaa kutokana na mizozo, mabadiliko ya tabia nchi na janga la Covid-19.

David Beasley ametoa wito kwa wahisani kusaidia kukabiliana na hali hiyo.Mkuu huyo wa shirika la mpango wa chakula duniani ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa kufanyiwa kazi onyo alilolitoa miezi mitano iliyopita kumesaidia kuzuia janga la njaa.

Beasley amesema shirika la WFP na washirika wake wamejaribu kuwafikia watu milioni 138 mwaka huu, idadi hiyo ikiwa kiwango kikubwa cha watu kusaidiwa katika historia na shirika hilo.

Hata hivyo ameonya kuwa watu milioni 270 wanakabiliwa na njaa. Tayari watu milioni 30 wanategemea chakula kutoka WFP na huenda wakafariki iwapo watakosa msaada huo.

Mataifa ambayo watu wake wanakabaliwa na njaa ni Congo, Yemen, Sudan Kusini na Nigeria.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *