WFP: Ulimwengu usilisahau eneo la Sahel,

October 10, 2020

Mtendaji Mkuu wa Shirika la Chaku Duniani, WFP David Beasley amesema kushinda Tuzo ya Amani ya Nobel wakati akiwasili katika eneo duni na kudhoofishwa kwa vita la Sahel, ni ujumbe kwa ulimwengu kwamba eneo hilo halipaswi kusahauliwa. 

Akizungumza na waandishi wa habari nchini Burkinafaso Beasley hapo jana, ukiwa muda mfupi tu, baada ya shirika hilo kushinda tuzo hiyo kutokana na kukabiliana na njaa katika kipindi ambacho mamilioni ya watu wanasukumwa katika wimbo la njaa kutokana na janga la corona, alisema kwa uhakika alipokea taarifa ya tuzo akiwa katika eneo la Sahel. 

Aidha yeye binafsi amonesha kusikitishwa kwake na hali ilivyo Burkinafaso, ambako makundi ya wanamgambo yanadhibiti maeneo kadhaa yenye kuhudumia watu na hivyo kufanya mamilioni ya watu kusalia na njaa. 

Zaidi ya watu milioni tatu nchini humo wanahitaji msaada wa dharura wa chakula na wengine 11,000 wapo katika mazingira ya njaa.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *