Wenye mrengo mkali wa kulia washambulia bunge la Ujerumani, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 2), on August 30, 2020 at 7:00 am

August 30, 2020

Polisi nchini Ujerumani walifanikiwa kuwazuia watu wenye itikadi kali za mrengo wa kulia waliotaka kulivamia jengo la bunge hapo jana Jumamosi.Kundi la waandamanaji hao walioondolewa kutoka eneo hilo walikuwa wanapinga vizuizi vya kukabiliana na janga la corona.Maelfu ya watu walihudhuria maandamano hayo yaliodumu kwa siku nzima kupinga kuvaa barakoa na taratibu nyingine zenye lengo la kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona.Polisi iliwaamuru waandamanaji kutawanyika katika mikusanyiko yao katika maeneo ya jiji la Berlin baada ya kushindwa kutekeleza kanuni ya kujitenga, lakini mkusanyiko uliopangwa kufanyika katika lango la kihistoria la Brandenburg uliendelea kama kawaida.Polisi inasema takribani watu 300 wametiwa mbaroni kufuatia ghasia hizo za maandamano hayo ambayo yalijumisha takribani watu 38,000.,

Polisi nchini Ujerumani walifanikiwa kuwazuia watu wenye itikadi kali za mrengo wa kulia waliotaka kulivamia jengo la bunge hapo jana Jumamosi.

Kundi la waandamanaji hao walioondolewa kutoka eneo hilo walikuwa wanapinga vizuizi vya kukabiliana na janga la corona.

Maelfu ya watu walihudhuria maandamano hayo yaliodumu kwa siku nzima kupinga kuvaa barakoa na taratibu nyingine zenye lengo la kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona.

Polisi iliwaamuru waandamanaji kutawanyika katika mikusanyiko yao katika maeneo ya jiji la Berlin baada ya kushindwa kutekeleza kanuni ya kujitenga, lakini mkusanyiko uliopangwa kufanyika katika lango la kihistoria la Brandenburg uliendelea kama kawaida.

Polisi inasema takribani watu 300 wametiwa mbaroni kufuatia ghasia hizo za maandamano hayo ambayo yalijumisha takribani watu 38,000.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *