Wenje ahaidi kila shule ya sekondari wilayani Rorya kuwa na Hosteli ya wasichana, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on September 3, 2020 at 1:00 pm

September 3, 2020

Na Timothy Itembe Mara.MGOMBEA Ubunge jimbo la Rorya kupitia tiketi ya Chama cha Demokorasia na Maendeleo Chadema ,Ezekiel Wenje amesema kuwa kama akipitishwa na kuwa Mbunge wa jimbo hilo atahakikisha kila shule ya sekondari wilayani humo inakuwa na Hosteli ya wasichana ili kuepusha mimba zisizotarajiwa.Wenje alisema hayo jana  wakati akiomba kura kwenye mkutano wa mkutano wa hadhara wa kampeni za Uzinduzi    uliofanyika, ndani ya viwanja vya kijiji cha Bututi kata ya Rablwo wilayani hapo .“Kama wananchi mkinichagua na kuwa  Mbunge wa jimbo la Rorya nitahakikisha kuwa kila shule ya sekondari wilayani hapa inakuwa na hosteli ili kuokoa wanafunzi wa kike  kupachikwa  mimba  zisizotarajiwa   mashuleni”alisema Wenje.Mgombea huyo aliongeza kuwa wananchi wa Rorya kuna haja ya kumwamini na kumchagua ili kuwa Mbunge wao ili kuwatumikia na kuwaletea maendeleo ndani ya jimbo la Rorya.Wenje aliongeza kuwa pamoja na kuanza na hosteli ya wasichana wa shule za sekondari atahakikisha miundombinu ya Barabara inaboreshwa na wananchi wanasafiri  kwa raha na kwa gharama na fuu.Naye Mgombea Udiwani ndani ya  kata ya Kitembe kupitia Chama cha Chadema,Thomas Rissa Patirrck  alimuomba Mgombea huyo kuwasaidia watu wa Rorya kuondokana na wizi wa Mifugo endapo atafanikiwa kuchaguliwa na kuwa Mbunge wao.Rissa aliongeza kuwa yeye binafsi anatetea nafasi yake ndani ya Kata ya kitembe na kuwa wakati akiwa Diwani alipambana na wizi wa mifogo na watu wa Rorya kwasasa wana ahuweni wanalala licha ya kuwa bado kuna harufu ya wizi wa mifugo Rorya.Mgombea udiwani huyo aliongeza kuwa wakati akipambana na wizi wa mifugo wakati mwingine alitumia gharama zake za mfukoni kuhakikisha kuwa watuhumiwa wa wizi wa mifugo wanakamatwa na kufiikishwa eneo husika pamoja na mifugo iliyoibwa inapatikana na kurudishwa  kwa wenyewe.           Rissa aliongeza kuwa ukitaja maendeleo ya Rorya ikiwemo kusomesha watoto hutakosa kutaja zao  la mifugo ambalo lina mchango mkubwa katika halmashauri hiyo kwa maendeleo yake lakini zao hilo linakumbwa na wizi wa mifugo.  ,

Na Timothy Itembe Mara.

MGOMBEA Ubunge jimbo la Rorya kupitia tiketi ya Chama cha Demokorasia na Maendeleo Chadema ,Ezekiel Wenje amesema kuwa kama akipitishwa na kuwa Mbunge wa jimbo hilo atahakikisha kila shule ya sekondari wilayani humo inakuwa na Hosteli ya wasichana ili kuepusha mimba zisizotarajiwa.

Wenje alisema hayo jana  wakati akiomba kura kwenye mkutano wa mkutano wa hadhara wa kampeni za Uzinduzi    uliofanyika, ndani ya viwanja vya kijiji cha Bututi kata ya Rablwo wilayani hapo .

“Kama wananchi mkinichagua na kuwa  Mbunge wa jimbo la Rorya nitahakikisha kuwa kila shule ya sekondari wilayani hapa inakuwa na hosteli ili kuokoa wanafunzi wa kike  kupachikwa  mimba  zisizotarajiwa   mashuleni”alisema Wenje.

Mgombea huyo aliongeza kuwa wananchi wa Rorya kuna haja ya kumwamini na kumchagua ili kuwa Mbunge wao ili kuwatumikia na kuwaletea maendeleo ndani ya jimbo la Rorya.

Wenje aliongeza kuwa pamoja na kuanza na hosteli ya wasichana wa shule za sekondari atahakikisha miundombinu ya Barabara inaboreshwa na wananchi wanasafiri  kwa raha na kwa gharama na fuu.

Naye Mgombea Udiwani ndani ya  kata ya Kitembe kupitia Chama cha Chadema,Thomas Rissa Patirrck  alimuomba Mgombea huyo kuwasaidia watu wa Rorya kuondokana na wizi wa Mifugo endapo atafanikiwa kuchaguliwa na kuwa Mbunge wao.

Rissa aliongeza kuwa yeye binafsi anatetea nafasi yake ndani ya Kata ya kitembe na kuwa wakati akiwa Diwani alipambana na wizi wa mifogo na watu wa Rorya kwasasa wana ahuweni wanalala licha ya kuwa bado kuna harufu ya wizi wa mifugo Rorya.

Mgombea udiwani huyo aliongeza kuwa wakati akipambana na wizi wa mifugo wakati mwingine alitumia gharama zake za mfukoni kuhakikisha kuwa watuhumiwa wa wizi wa mifugo wanakamatwa na kufiikishwa eneo husika pamoja na mifugo iliyoibwa inapatikana na kurudishwa  kwa wenyewe.           

Rissa aliongeza kuwa ukitaja maendeleo ya Rorya ikiwemo kusomesha watoto hutakosa kutaja zao  la mifugo ambalo lina mchango mkubwa katika halmashauri hiyo kwa maendeleo yake lakini zao hilo linakumbwa na wizi wa mifugo.  

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *