Wenger: Nilipewa ofa ya kuifundisha Man United,

October 3, 2020

 

kocha wa zamani wa Arsenal mfaransa Arsene Wenger amesema alipewa ofa ya kuifundisha Manchester United.

Wenger alikuwa kocha wa Arsenal kwa kipindi cha miaka 22, kuanzia mwaka 1996 mpaka 2018 ambapo alishinda jumla ya mataji 17 akiwa na kikosi hicho cha washika bunduki wa jiji la London ukiwemo ubingwa wa ligi kuu England EPL mara tatu na ubingwa wa kombe la FA mara saba.

Kocha huyo amesema alipewa ofa ya kujiunga na Manchester United wakati bado akiwa na kikosi cha Arsenal. baada ya kuulizwa kama aliwahi kupewa ofa ya kuinoa Man Utd alijibu

“Ndio,ila siwezi kukwambia ofa hiyo nilipewa lini, lakini nakwambia Man United walinipa ofa”

Inaripotiwa kuwa msimu wa 2000-2001 ndio msimu ambao Manchester United walitaka kumchukua Wenger kama mbadala wa kocha Sir Alex Ferguson ambaye alikuwa na mpango wa kustaafu msimu huo kabla ya kubadili mawazo yake na kusalia kwa miaka 12 zaidi.

Arsene Wenger pia ameweka wazi kuwa sio Man United pekee ambao walionyesha nia ya kuhitaji huduma yake lakini hata vilabu vya Bayern Munich ya Ujerumani, Real Madrid na Barcelona za Hispania, Juventus ya Italia, klabu ya PSG ya Ufaransa nayo ilishampa ofa ya kukinoa kikosi hicho zaidi ya mara moja na ofa nyingine ilikuwa kutoka timu ya taifa ya Ufaransa.

Kwa sasa Wenger hana timu anayoifundisha toka alivyoachana na kikosi cha Arsenal mwaka 2018, licha ya kuwa na umri wa miaka 70 mfaransa huyo bado hajatangaza kustaafu.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *