Waziri wa zamani wa mambo ya ndani wa Italia afikishwa mahakamani kutokana na kuzuia meli za uokozi,

October 3, 2020

Mwanasiasa wa mrengo wa kulia na waziri wa zamani wa mambo ya ndani wa Italia, Matteo Salvini leo amefikishwa mbele ya mahakama moja ya kisiwa cha Sicily itakayoamua iwapo ana kesi ya kujibu baada ya mwaka 2019 kuwazuia kwa siku kadhaa wahamiaji 131 waliokolewa baharini na meli ya walinzi wa pwani. 


Hatua hiyo inafuatia kura iliyopigwa na baraza la seneti mwezi Februari ya iliyomuondolea kinga mwanasiasa huyo na kufungua milango ya kushtakiwa kwa makosa ya utekaji nyara na matumizi mabaya ya madaraka. 

Katika kisa cha Julai mwaka 2019 meli ya uokozi iitwayo Gregoretti ilikwama kwa siku kadhaa baharini baada ya Salvini kuizuia kutia nanga kwenye bandari za Italia hadi mahakama ilipotoa amri ya kuondoa zuia hilo. 

Wakati wa muhula wake wa miezi 14 kama waziri wa mambo ya ndani wa Italia, Salvini alikataa kutoa idhini ya kutia nanga kwa meli zinazowaokoa wahamiaji uamuzi uliolazimisha wahamiaji kubakia baharini kwa wiki kadhaa.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *