Waziri wa Ulinzi wa zamani wa Mexico akamatwa Marekani,

October 17, 2020

Waziri wa zamani wa Ulinzi wa Mexico, Salvador Cienfuegos, ametiwa mbaroni nchini Marekani kwa tuhuma za utapeli wa fedha na ulanguzi wa madawa ya kulevya.

Kwa mujibu wa vyanzo vya Marekani na Mexico, Salvador Cienfuegos mwenye umri wa miaka 72 ambaye alihudumu kama Waziri wa Ulinzi wa serikali ya rais Enrique Pena Nieto kati ya mwaka 2012-2018, alikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Los Angeles kufuatia agizo la idara ya kukabiliana na madawa ya kulevya nchini Marekani DEA.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Mexico Marcelo Ebrard alitoa maelezo kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter na kusema kuwa alimfahamisha balozi wa Marekani Christopher Landau kuhusu hali ya jenerali mstaafu na kumhakikishia haki ya kuomba msaada kwa ubalozi.

Kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa Mexico ambaye hakutaka kudhihirishwa jina, alifahamisha kuwa alikuwepo karibu na familia ya Cienfuegos baada ya tukio hilo.

Idara ya kukabiliana na madawa ya kulevya nchini Marekani DEA, haijatoa maelezo yoyote kuhusu tukio hilo.

Jeshi la Mexico lilikuwa likishutumiwa mara nyingi kwa ukiukaji wa haki za kibinadamu wakati Cienfuegos alipokuwa akihudumu kama Waziri wa Ulinzi.

Kashfa kubwa zaidi ya kipindi cha Cienfuegos ilikuwa ni mwaka 2014 ambapo wanajeshi walitekeleza mauaji ya washukiwa 22 kwenye ghala ya Tlatlaya.

Uchunguzi wa haki za binadamu ulibaini kuwa washukiwa wasiopungua 8 waliuawa baada ya kujisalimisha.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *