Waziri wa Ulinzi wa Azerbaijan na Uturuki wazungumza,

October 17, 2020

 

Waziri wa Ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar amesema kuwa Armenia inaendelea kufanya uhalifu wa kivita, na wale wanaotaka kusitishwa kwa mapigano na mazungumzo wanaendelea kufuatilia mashambulizi hayo kutoka mbali.

Katika mazungumzo ya simu ya Hulusi Akar na Waziri wa Ulinzi wa Azerbaijan Zakir Hasanov, mapigano na Armenia yalijadiliwa.

Akar, akipongeza Jeshi la Azerbaijan ambalo lilifanikiwa kuitungua ndege ya kivita ya Armenia SU-25 kabla ya ndege hiyo kutekeleza mashambulizi amesema,

“Armenia inaendelea kufanya uhalifu wa kivita, wale ambao wanataka kusitisha mapigano na mazungumzo wanaendelea kufuatilia mashambulizi hayo kutoka mbali.”

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *