Waziri wa Uganda kushitakiwa kufuatia kisa cha ufyatulianaji risasi, on September 7, 2020 at 8:00 am

September 7, 2020

Waziri wa leba wa Uganda, Mwesigwa Rukutana, anatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatatu baada ya kukamatwa kufuatia kisa cha ufyatulianaji risasi.Waziri huyo anadaiwa kumpiga risasi mfuasi wa mpinzani wake baada ya kushindwa katika uchaguzi wa chama tawala cha National Resistance Movement (NRM).Mfuasi mmoja alijeruhiwa vibaya na wengine wawili kupata majeraha madogo, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari nchini humo.Bwana Rukutana amekanusha madai ya kuwafyatulia risasi wafuasi wa mpinzani wake.Vyombo vya habari vimemnukuu mmoja wa watu walioshuhudia kisa hicho akisema waziri alichukua bunduki kutoka kwa mmoja wa walinzi na kuanza kuwapiga risasi wafuasi wa mpinzani wake.Waziri huyo pamoja na walinzi wake watatu walitiwa nguvuni.Watashitakiwa kwa jaribio la mauaj, kwa mujibu wa naibu wa msemaji wa polisi Polly Namaye.,

Waziri wa leba wa Uganda, Mwesigwa Rukutana, anatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatatu baada ya kukamatwa kufuatia kisa cha ufyatulianaji risasi.

Waziri huyo anadaiwa kumpiga risasi mfuasi wa mpinzani wake baada ya kushindwa katika uchaguzi wa chama tawala cha National Resistance Movement (NRM).

Mfuasi mmoja alijeruhiwa vibaya na wengine wawili kupata majeraha madogo, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari nchini humo.

Bwana Rukutana amekanusha madai ya kuwafyatulia risasi wafuasi wa mpinzani wake.

Vyombo vya habari vimemnukuu mmoja wa watu walioshuhudia kisa hicho akisema waziri alichukua bunduki kutoka kwa mmoja wa walinzi na kuanza kuwapiga risasi wafuasi wa mpinzani wake.

Waziri huyo pamoja na walinzi wake watatu walitiwa nguvuni.

Watashitakiwa kwa jaribio la mauaj, kwa mujibu wa naibu wa msemaji wa polisi Polly Namaye.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *