Waziri wa Sierra Leone amesimamishiwa kazi juu ya ufisadi,

October 6, 2020

Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio amewasimamisha kazi watumishi wa umma waliotajwa kwenye ripoti iliyoangazia ufisadi.

Walioathirika ni pamoja na waziri wa kilimo Dennis Vandi na katibu makamu rais, Baba Fortune.

Ripoti hiyo inayoangazia ufisadi iliyotolewa na tume maalum ya kuchunguza kubaini ukweli wa mambo imewahusisha watu kadhaa waliokuwa watumishi wa umma na wa sasa na wizi wa fedha za umma.

Waziri Vandi amesema kwamba yeye hana hatia na hakupewa fursa na tume hiyo ya kujitetea.

Wote waliotajwa wamepewa miezi mitatu kukata rufaa.

Baadhi ya waliokuwa mawaziri na maafisa kadhaa wamepigwa marufuku kuondoka nchini humo juu ya madai ya ufisadi.

Aidha, aliyekuwa rais, Ernest Bai Koroma, yuko kwenye orodha ya watu 102 waliohusishwa na madai ya ufisadi yaliyochapishwa na gazeti la Sierra Leone Telegraph.

Rais Bio ameahidi kurejesha pesa zinazodaiwa kufunjwa na mtangulizi wake.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *