Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani kufanya ziara nchini Uturuki wiki ijayo,

October 10, 2020

Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas, anatarajia kufanya ziara nchini Uturuki wiki ijayo.

Ujerumani inaendelea na jukumu la upatanishi Mediterania kati ya Uturuki na Ugiriki.

Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas anatarajiwa kufanya ziara katika mji mkuu Ankara Jumatano, Oktoba 14 na kukutana na Waziri wa Mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu.

Wakati wa ziara hiyo, inategemewa kuwa uhusiano wa nchi mbili na maendeleo ya kikanda, haswa Mashariki ya Mediterania, ni mada zitakazojadiliwa.

Heiko Maas amesema baada ya Uturuki atatembelea Athene na Nicosia.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *