Waziri wa mambo ya ndani mwenye nguvu Libya aachishwa kazi kutokana na maandamano, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on August 29, 2020 at 1:00 pm

August 29, 2020

Kiongozi wa serikali ya Libya inayotambulika kimataifa Fayez al Sarraj amemsimamisha kazi waziri wake wa mambo ya ndani mwenye nguvu Fathi Bashagha, akisema kuwa atafanyiwa uchunguzi wa namna alivyoyashughulikia maandamano na ukandamizaji dhidi ya waandamanaji. Hatua hiyo inakwenda sanjari na ripoti za kuongezeka mvutano kati ya waziri mkuu na waziri huyo, ambaye ni kiongozi mwenye ushawishi mkubwa kutokea mji wa bandari na ngome ya kijeshi ya Misrata. Bashagha, aliyeteuliwa mwaka wa 2018, alikuwa na mchango mkubwa katika operesheni ya miezi 14 ya wanajeshi wa serikali pinzani ya mashariki ya kuukamata mji mkuu Tripoli ambayo serikali ya Tripoli iliizuia kwa msaada wa kijeshi kutoka Uturuki. Amri iliyotolewa na Sarraj ilisema Bashagha atachunguzwa na uongozi wa serikali katika masaa 72, na majukumu yake yatachukuliwa na naibu waziri, Khalid Ahmad Mazen. Bashagha amesema yuko tayari kwa uchunguzi, lakini uonyeshwe moja kwa moja na televisheni ili kuhakikisha uwazi.,

Kiongozi wa serikali ya Libya inayotambulika kimataifa Fayez al Sarraj amemsimamisha kazi waziri wake wa mambo ya ndani mwenye nguvu Fathi Bashagha, akisema kuwa atafanyiwa uchunguzi wa namna alivyoyashughulikia maandamano na ukandamizaji dhidi ya waandamanaji.

 Hatua hiyo inakwenda sanjari na ripoti za kuongezeka mvutano kati ya waziri mkuu na waziri huyo, ambaye ni kiongozi mwenye ushawishi mkubwa kutokea mji wa bandari na ngome ya kijeshi ya Misrata. 

Bashagha, aliyeteuliwa mwaka wa 2018, alikuwa na mchango mkubwa katika operesheni ya miezi 14 ya wanajeshi wa serikali pinzani ya mashariki ya kuukamata mji mkuu Tripoli ambayo serikali ya Tripoli iliizuia kwa msaada wa kijeshi kutoka Uturuki. 

Amri iliyotolewa na Sarraj ilisema Bashagha atachunguzwa na uongozi wa serikali katika masaa 72, na majukumu yake yatachukuliwa na naibu waziri, Khalid Ahmad Mazen. Bashagha amesema yuko tayari kwa uchunguzi, lakini uonyeshwe moja kwa moja na televisheni ili kuhakikisha uwazi.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *