waziri wa habari wananchi wapewe Elimu, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on August 29, 2020 at 1:00 pm

August 29, 2020

Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo ameitaka jamii kupatiwa elimu ya mazingira ili wawe  na utaratibu wa kuweka  usafi katika mazingira wanayoishi.Wito huo ameutoa huko Mbweni wakati alipokuwa akizungumza na vikundi vya usafishaji vya WAJAMAMA ambayo ni kampuni inayoweka akinamama na watoto katika hali ya usafi na kuwa na afya bora  wakishirikiana  na Safisha Zanzibar  kwa lengo la kuona mji unakuwa safi na unavutia .Amesema jamii inaona labda usafi ni wa Serikali peke yake au manispaa  dhana hiyo indoshwe kwani kila binaadamu au kiumbe chochote kinahitaji kuwa na mazingira ya usafi sehemu anayoishi hivyo jitihada za kutoa elimu zinahitajika zaidi.Hata hivyo amesema iwapo usafi utakuwemo nchini maradhi ya mripuko hayataweza kutokea Bajeti ya dawa itapungua  uchumi utaongezeka    kwa sababu wananchi watakuwa na afya nzuri na hilo ndio  lengo la Serikali.”Iwapo usafi utadumishwa jamii itaishi kwa kuwa na afya njema itaepukana na maradhi ya mripuko na ndio azma ya Serikali yetu”, alisema Waziri huyo.Aidha amesema mji unapokuwa safi mazingira yanapendeza  hata watalii wataongezeka vijana watapata ajira na pato la Serikali litaongezeka.,

Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo ameitaka jamii kupatiwa elimu ya mazingira ili wawe  na utaratibu wa kuweka  usafi katika mazingira wanayoishi.

Wito huo ameutoa huko Mbweni wakati alipokuwa akizungumza na vikundi vya usafishaji vya WAJAMAMA ambayo ni kampuni inayoweka akinamama na watoto katika hali ya usafi na kuwa na afya bora  wakishirikiana  na Safisha Zanzibar  kwa lengo la kuona mji unakuwa safi na unavutia .

Amesema jamii inaona labda usafi ni wa Serikali peke yake au manispaa  dhana hiyo indoshwe kwani kila binaadamu au kiumbe chochote kinahitaji kuwa na mazingira ya usafi sehemu anayoishi hivyo jitihada za kutoa elimu zinahitajika zaidi.

Hata hivyo amesema iwapo usafi utakuwemo nchini maradhi ya mripuko hayataweza kutokea Bajeti ya dawa itapungua  uchumi utaongezeka    kwa sababu wananchi watakuwa na afya nzuri na hilo ndio  lengo la Serikali.

“Iwapo usafi utadumishwa jamii itaishi kwa kuwa na afya njema itaepukana na maradhi ya mripuko na ndio azma ya Serikali yetu”, alisema Waziri huyo.

Aidha amesema mji unapokuwa safi mazingira yanapendeza  hata watalii wataongezeka vijana watapata ajira na pato la Serikali litaongezeka.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *