Waziri wa Columbia aomba msamaha huku maandamano dhidi ya ukatili wa polisi yakiendelea, on September 12, 2020 at 10:00 am

September 12, 2020

Waziri wa ulinzi wa Colombia Carlos Holmes Trujillo ameomba msamaha kwa niaba ya idara ya polisi kwa kifo cha mwanamume mmoja aliyeuawa katika kizuizi cha polisi ambacho kimechochea maandamano ya siku kadhaa mjini Bogota na mji jirani wa Soacha na kusababisha vifo vya watu 13 na mamia ya wengine kujeruhiwa.Rais wa nchi hiyo Ivan Duque amesema jana kuwa vifo vyote hivyo vitachunguzwa na hakuna ukiukaji wa vikosi vya usalama utakaovumiliwa.Waandamanaji wameandamana kwa siku kadhaa kulalamika kuhusu kifo cha Javier Oronez wa umri wa miaka 46 kilichotokea siku ya Jumatano.Idara ya polisi imesema kuwa Ordonez alipatikana akinywa pombe barabara na rafiki zake na kukiuka sheria ya kudumisha umbali wa mtu mmoja hadi mwingine kuzuia kuenea kwa virusi vya corona. Maafisa wawili waliohusishwa na kifo cha Ordonez wamefutwa kazi na wanakabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya mamlaka na mauaji.,

Waziri wa ulinzi wa Colombia Carlos Holmes Trujillo ameomba msamaha kwa niaba ya idara ya polisi kwa kifo cha mwanamume mmoja aliyeuawa katika kizuizi cha polisi ambacho kimechochea maandamano ya siku kadhaa mjini Bogota na mji jirani wa Soacha na kusababisha vifo vya watu 13 na mamia ya wengine kujeruhiwa.

Rais wa nchi hiyo Ivan Duque amesema jana kuwa vifo vyote hivyo vitachunguzwa na hakuna ukiukaji wa vikosi vya usalama utakaovumiliwa.Waandamanaji wameandamana kwa siku kadhaa kulalamika kuhusu kifo cha Javier Oronez wa umri wa miaka 46 kilichotokea siku ya Jumatano.

Idara ya polisi imesema kuwa Ordonez alipatikana akinywa pombe barabara na rafiki zake na kukiuka sheria ya kudumisha umbali wa mtu mmoja hadi mwingine kuzuia kuenea kwa virusi vya corona.

 Maafisa wawili waliohusishwa na kifo cha Ordonez wamefutwa kazi na wanakabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya mamlaka na mauaji.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *