Waziri Mkuu wa Uingereza na Mkuu wa Umoja wa Ulaya kufanya mazungumzo ya Brexit,

October 2, 2020

 

Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen atafanya mazungumzo kupitia njia ya video na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson hapo kesho katika juhudi za kutafuta maelewano katika majadiliano ya baada ya Uingereza kujiondoa kutoka kwenye Umoja wa Ulaya, Brexit. 

Msemaji wa von der Leyer Eric Mamer ameandika katika mtandao wa kijamii wa twitter kuwa viongozi hao wawili watakutana mchana na Uingereza nayo ikathibitisha mazungumzo hayo. 

Viongozi wa majadiliano hayo kutoka Umoja wa Ulaya na Uingereza Michel Barnier na David Frost wanakutana mjini Brussels leo kwa ajili ya duru ya mwisho ya mazungumzo hayo ila hakutarajiwi makubaliano ya aina yoyote ile.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *