Waziri Mkuu wa Ubelgiji atoa wito kwa upinzani kumaliza tofauti,

October 3, 2020

 

Waziri Mkuu mpya wa Ubelgiji, Alexander De Croo leo ametoa wito kwa upande wa upinzani kumaliza tofauti zilizopo na kufanya kazi pamoja ili kuliendeleza taifa hilo la Ulaya Magharibi. 

Kulingana na shirika la habari la Belga, De Croo amesema hadhani kuwa upinzani umetengwa katika mipango na malengo ya serikali mpya. 

Muungano wa vyama vya kiliberali nchini Ubelgiji ulichukua hatamu za uongozi Alhamisi iliyopita baada ya vyama saba kufikia makubaliano ya kuunda serikali miezi 16 baada ya uchaguzi. 

Moja ya vipaumbele muhimu vya serikali hiyo ni kukabiliana na janga la virusi vya corona na kufufua tena uchumi wa Ubelgiji baada ya miezi kadhaa ya vizuizi vikali vya kukabiliana na janga la virusi hivyo. 

Hadi sasa visa vya Covid-19 vinaendelea kupanda nchini Ubelgiji huku vifo vilivyotokana na ugonjwa huo vikipindukia watu 10,000 kwenye taifa hilo lenye wakaazi milioni 11.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *