Waziri mkuu wa Lebanon kuunda serikali ndani ya wiki mbili, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 2), on September 2, 2020 at 6:00 pm

September 2, 2020

Waziri mkuu mteule wa Lebanon Mustapha Idib leo ameamzisha mazungumzo ya kuunda serikali itakayoshughulikia utatuzi wa mgogoro, chini ya shinikizo la Ufaransa kuhitimisha jukumu hilo ndani ya wiki mbili, ili kuendelea mbele na mageuzi muhimu yanayohitajika.Mashauriano hayo yanafuatia ziara ya ngazi ya juu kabisa ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambapo katika safari hiyo alisema viongozi wa kisiasa wamekubali muongozo wa kisiasa kwa ajili ya mabadiliko baada ya mripuko mbaya wa mwezi uliopita katika bandari ya Beirut.Waziri Mkuu Adib ameanza kukutana na viongozi wa bunge katika kipindi hiki ambacho pia Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis akionya kwamba Lebanon inakabiliwa na hatari ambayo inatishia hata uwepo wa taifa hilo. Papa alisema Lebanon haiwezi kuachwa peke yake.,

Waziri mkuu mteule wa Lebanon Mustapha Idib leo ameamzisha mazungumzo ya kuunda serikali itakayoshughulikia utatuzi wa mgogoro, chini ya shinikizo la Ufaransa kuhitimisha jukumu hilo ndani ya wiki mbili, ili kuendelea mbele na mageuzi muhimu yanayohitajika.

Mashauriano hayo yanafuatia ziara ya ngazi ya juu kabisa ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambapo katika safari hiyo alisema viongozi wa kisiasa wamekubali muongozo wa kisiasa kwa ajili ya mabadiliko baada ya mripuko mbaya wa mwezi uliopita katika bandari ya Beirut.

Waziri Mkuu Adib ameanza kukutana na viongozi wa bunge katika kipindi hiki ambacho pia Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis akionya kwamba Lebanon inakabiliwa na hatari ambayo inatishia hata uwepo wa taifa hilo. Papa alisema Lebanon haiwezi kuachwa peke yake.,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *