Waziri Mkuu mpya wa Japan kuchaguliwa Septemba, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on August 31, 2020 at 3:00 pm

August 31, 2020

Ni siku chache baada ya Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe, kutangaza kujiuzulu kutoka kwenye wadhfa wake kutokana na matatizo ya kiafya.Shinzo alitangaza kujiuzulu kwake na kusema kuwa hakutaka ugonjwa wake uathiri kwa namna moja ama nyingine uamuzi wake wowote wa kisiasa.Kwa sasa Japan inatarajia kuchagua Waziri wake mpya katika kikao cha bunge kinachotarajiwa kufanyika mnamo 17 mwezi Septemba.Kulingana na kituo cha habari cha taifa NHK, chama kilichopo madarakani LDP kitatangaza ratiba rasmi ya uchaguzi wa kiongozi atakayechukua nafasi ya Shinzo Abe.Kati ya viongozi wanaotarajia kushiriki katika kin’gan’ganyiro hicho ni Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa taifa hilo Kishida Fumio na Waziri wa zamani wa Ulinzi Isiba Shigeru.,

Ni siku chache baada ya Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe, kutangaza kujiuzulu kutoka kwenye wadhfa wake kutokana na matatizo ya kiafya.

Shinzo alitangaza kujiuzulu kwake na kusema kuwa hakutaka ugonjwa wake uathiri kwa namna moja ama nyingine uamuzi wake wowote wa kisiasa.

Kwa sasa Japan inatarajia kuchagua Waziri wake mpya katika kikao cha bunge kinachotarajiwa kufanyika mnamo 17 mwezi Septemba.

Kulingana na kituo cha habari cha taifa NHK, chama kilichopo madarakani LDP kitatangaza ratiba rasmi ya uchaguzi wa kiongozi atakayechukua nafasi ya Shinzo Abe.

Kati ya viongozi wanaotarajia kushiriki katika kin’gan’ganyiro hicho ni Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa taifa hilo Kishida Fumio na Waziri wa zamani wa Ulinzi Isiba Shigeru.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *