Waziri Kabudi Aruhusiwa Kutoka Hospitali

October 15, 2020

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, ameruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu baada ya kupata ajali jana, Oktoba 14, 2020.

Ajali hiyo ilitokea eneo la Kihonda, Manispaa ya Morogoro katika barabara kuu ya Dodoma-Morogoro, chanzo  kikidaiwa kuwa ni dereva wa Bajaj kuchomekea mbele ya gari la waziri huyo ghafla.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *