Waziri Kabudi Apata Ajali

October 14, 2020

Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amepata ajali ya gari mkoani Morogoro leo Jumatano tarehe 14 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).

Akizungumza nje ya Hospitali ya Rufaa ya Morogoro, Mkuu wa Mkoa huo, Loata Sanare amesema, leo walikuwa na ziara wilayani Kilosa na tayari walikwisha kufika lakini baadaye walipata taarifa  Waziri Kabudi amepata ajali.

 

Kabudi naye alikuwa anakwenda Kilosa ambako yeye ni mbunge mteule wa Jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Madaktari wamemcheki hana tatizo kubwa sana, anahitaji kupumzika. Niwatoe wasiwasi  wana Kilosa na Watanzania, Mzee Kabudi amepata ajali lakini anaendelea vizuri,” amesema.

Sanare amesema, baada ya mapumziko aliyopewa Waziri Kabudi, watapata maelekezo mengine ya nini cha kufanya.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *