Waziri Hasunga awashushia neema wakulima wa kahawa Karagwe na Kyerwa, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 2), on September 3, 2020 at 5:00 pm

September 3, 2020

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga Leo tarehe 3 Septemba 2020 amewasili Wilayani Karagwe katika mkoa wa Kagera kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, ambapo amekagua shughuli mbalimbali za kilimo.Katika ziara hiyo Waziri Hasunga amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa vyama vya Ushirika (AMCOS) wa Wilaya ya Kyerwa na Karagwe ambapo amejionea hali ya malipo ya wakulima wa kahawa wanaodai.Waziri Hasunga amekiagiza Chama Kikuu cha Ushirika Karagwe (KDCU) kuwalipa wakulima malipo yao ambapo ametoa siku tatu kuanzia tarehe 4 Septemba 2020 mpaka Septemba 6, 2020 Jumla ya Bilioni 7.8 ziwe zimelipwa haraka.“Ninyi KDCU ndio mmechukua kahawa za wakulimaa mmechukua kwa malikauli wananchi wakawaamini na kuwapa kahawa lakini mkawapa maneno mazuri kwamba mtawalipa kwa wakati lakini mmeshindwa kuwalipa mpaka sasa” Amesisitiza Waziri Hasunga.Ametoa maagizo hayo mbele ya Kamati ya ulinzi na usalama pamoja na wataalamu wa Wilaya ya Karagwe huku akikitaka Shirika la ukaguzi wa hesabu za vyama vya Ushirika (COASCO) kukamilisha ukaguzi wa vyama vya Ushirika ndani ya wiki mbili ili wakulima waweze kulipwa fedha zao za malipo ya nyongeza, Kadhalika ameitaka COASCO kupitia hesabu zao ili waweze kutoa taarifa.Hasunga amesema kuwa ni Marufuku kuchelewesha malipo ya wakulima badala yake Bodi ya Kahawa kwa kushirikiana na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania inapaswa kubainisha njia bora ili kurahisisha malipo ya wakulima.Vilevile, Waziri Hasunga ameitaka Bodi ya kahawa kujenga maeneo maalumu kwa ajili ya kuhamasisha unywaji wa kahawa wa ndani kwani kufanya hivyo kutaongeza soko la ndani la kahawa.,

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga Leo tarehe 3 Septemba 2020 amewasili Wilayani Karagwe katika mkoa wa Kagera kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, ambapo amekagua shughuli mbalimbali za kilimo.

Katika ziara hiyo Waziri Hasunga amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa vyama vya Ushirika (AMCOS) wa Wilaya ya Kyerwa na Karagwe ambapo amejionea hali ya malipo ya wakulima wa kahawa wanaodai.

Waziri Hasunga amekiagiza Chama Kikuu cha Ushirika Karagwe (KDCU) kuwalipa wakulima malipo yao ambapo ametoa siku tatu kuanzia tarehe 4 Septemba 2020 mpaka Septemba 6, 2020 Jumla ya Bilioni 7.8 ziwe zimelipwa haraka.

“Ninyi KDCU ndio mmechukua kahawa za wakulimaa mmechukua kwa malikauli wananchi wakawaamini na kuwapa kahawa lakini mkawapa maneno mazuri kwamba mtawalipa kwa wakati lakini mmeshindwa kuwalipa mpaka sasa” Amesisitiza Waziri Hasunga.

Ametoa maagizo hayo mbele ya Kamati ya ulinzi na usalama pamoja na wataalamu wa Wilaya ya Karagwe huku akikitaka Shirika la ukaguzi wa hesabu za vyama vya Ushirika (COASCO) kukamilisha ukaguzi wa vyama vya Ushirika ndani ya wiki mbili ili wakulima waweze kulipwa fedha zao za malipo ya nyongeza, Kadhalika ameitaka COASCO kupitia hesabu zao ili waweze kutoa taarifa.

Hasunga amesema kuwa ni Marufuku kuchelewesha malipo ya wakulima badala yake Bodi ya Kahawa kwa kushirikiana na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania inapaswa kubainisha njia bora ili kurahisisha malipo ya wakulima.

Vilevile, Waziri Hasunga ameitaka Bodi ya kahawa kujenga maeneo maalumu kwa ajili ya kuhamasisha unywaji wa kahawa wa ndani kwani kufanya hivyo kutaongeza soko la ndani la kahawa.,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *