Wazee wa mila koo 13 kabila la Wakurya watoa tamko la kukipa chama cha mapinduzi kura, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on August 31, 2020 at 10:00 am

August 31, 2020

Na Timothy Itembe Mara.WAZEE wa mila muungano wa koo 13 kutoka kabila la Wakurya wilayani Tarime mkoani Mara wametoa tamko la kuunga mkono Serikali ya Chama cha mapinduzi CCM pamoja na mbombea  Ubunge Jimbo la Tarime Mjini,Michael Kembaki kwa lengo la kukipa kura zote za ndio chama cha mapinduzi. Nchagwa Motongori ambaye ni mwenyekiti wa muungano wa koo 13 kabila la Wakurya wilayani hapa alisema kuwa wazee hao kwa kauli moja wanaunga mkono wagombea wa Chama cha mapinduzi CCM kutokana na kutekeleza Ilani ya uchaguzi wa Chama hicho kwa miaka mitano iliyopita 2015-2020.Motongori aliongeza kuwa Lengo la kuunda umoja wa muungano wa koo 13 wa kabila la wakurya nikutokana na machafuko yaliyosababisha kukosekana Amani miaka ya nyuma ikiwemo mapigano ya koo hususani mapigano ya mwaka 2007 na kusababisha mauaji na mali za Watu kuporwa na kuharibiwa vibaya.Mzee huyo aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo ya kuunda umoja huo Tarime sasa kuna Amani na wazee hawatarajii tena kuona  Amani iliyopo  inavurugwa ambapo pia mzee huyo alitumia nafasi hiyo kuwaonya vijana kudumisha Amani hiyo na kuondokana kutumiwa na wanasiasa.Kwa upande wake Mgombea Ubunge jimbo la Tarime Mjini,Michael Kembaki aliomba wananchi kumpa kura zote za ndio kwa sababu ametekeleza Ahadi alizoahidi wakati akigombea mwaka 2015 licha ya kuwa kura hazikutosha na jimbo la Tarime Mjini kuongozwa na upinzani kwa maana ya Esther  Matiko kutoka Chama cha Demokorasia na maendeleo Chadema.Kembaki aliongeza kusema kuwa hatakuwa tayari kuona Jimbo linaenda upinzani kwa sababu amejipanga mwaka huu tofauti na mwaka wa uchaguzi uliopita 2015 na kuwa akichaguliwa atatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha mapinduzi kupitia ushirikiano wa Serikali na wananchi wa jimbo lake.“Licha ya kuwa kura hazikutosha mwaka 2015 ili kuwa Mbunge bado niliendelea kuchagia shuguli za maendeleo katika jimbo la Tarime mjini na viungo vyake kama nilivyokuwa nikiahidi wakati wa  kampeni,Nimekuwa  nikitumia fedha yangu ya mfukoni huku  ni kijinyima kula vizuri pamoja na watoto wangu ambapo fedha hiyo nimekuwa nikiitumia kutekeleza miradi kama vile  kujenga vyumba vya madarasa kwa baadhi ya shule za halmashauri ya mji”alisema Kembaki.Naye mwenekiti wa Chama cha mapinduzi mkoani hapa Samweli Keboye (NAMBA TATU) akimkabidhi Ilani ya uchaguzi  ya Chama cha mapinduzi mgombea huyo Namba tatu alisema kuwa kama Kembaki akifanikiwa na kuwa Mbunge ashugulikie ujenzi wa Soko ambalo olimebomolewa pamoja na kuleta maendeleo mengine kama vile  maji ambayo ni kero ndani ya Mji wa Tarime.Wakati huo huo Katibu wa Chama cha mapinduzi wilaya Tarime,Khamis Mkaruka aliomba wanachama kuvunja makundi yaliyokuwepo wakati wa watia nia ili kuwaunga mkono wagombea wa Chama cha mapinduzi akiwemo mgombea Urais John Pombe Magufuli Wabunge na madiwani wote wa Chama cha mapinduzi na kuwapa kura zote za ndio.,

Na Timothy Itembe Mara.

WAZEE wa mila muungano wa koo 13 kutoka kabila la Wakurya wilayani Tarime mkoani Mara wametoa tamko la kuunga mkono Serikali ya Chama cha mapinduzi CCM pamoja na mbombea  Ubunge Jimbo la Tarime Mjini,Michael Kembaki kwa lengo la kukipa kura zote za ndio chama cha mapinduzi.

 Nchagwa Motongori ambaye ni mwenyekiti wa muungano wa koo 13 kabila la Wakurya wilayani hapa alisema kuwa wazee hao kwa kauli moja wanaunga mkono wagombea wa Chama cha mapinduzi CCM kutokana na kutekeleza Ilani ya uchaguzi wa Chama hicho kwa miaka mitano iliyopita 2015-2020.

Motongori aliongeza kuwa Lengo la kuunda umoja wa muungano wa koo 13 wa kabila la wakurya nikutokana na machafuko yaliyosababisha kukosekana Amani miaka ya nyuma ikiwemo mapigano ya koo hususani mapigano ya mwaka 2007 na kusababisha mauaji na mali za Watu kuporwa na kuharibiwa vibaya.

Mzee huyo aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo ya kuunda umoja huo Tarime sasa kuna Amani na wazee hawatarajii tena kuona  Amani iliyopo  inavurugwa ambapo pia mzee huyo alitumia nafasi hiyo kuwaonya vijana kudumisha Amani hiyo na kuondokana kutumiwa na wanasiasa.

Kwa upande wake Mgombea Ubunge jimbo la Tarime Mjini,Michael Kembaki aliomba wananchi kumpa kura zote za ndio kwa sababu ametekeleza Ahadi alizoahidi wakati akigombea mwaka 2015 licha ya kuwa kura hazikutosha na jimbo la Tarime Mjini kuongozwa na upinzani kwa maana ya Esther  Matiko kutoka Chama cha Demokorasia na maendeleo Chadema.

Kembaki aliongeza kusema kuwa hatakuwa tayari kuona Jimbo linaenda upinzani kwa sababu amejipanga mwaka huu tofauti na mwaka wa uchaguzi uliopita 2015 na kuwa akichaguliwa atatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha mapinduzi kupitia ushirikiano wa Serikali na wananchi wa jimbo lake.

“Licha ya kuwa kura hazikutosha mwaka 2015 ili kuwa Mbunge bado niliendelea kuchagia shuguli za maendeleo katika jimbo la Tarime mjini na viungo vyake kama nilivyokuwa nikiahidi wakati wa  kampeni,Nimekuwa  nikitumia fedha yangu ya mfukoni huku  ni kijinyima kula vizuri pamoja na watoto wangu ambapo fedha hiyo nimekuwa nikiitumia kutekeleza miradi kama vile  kujenga vyumba vya madarasa kwa baadhi ya shule za halmashauri ya mji”alisema Kembaki.

Naye mwenekiti wa Chama cha mapinduzi mkoani hapa Samweli Keboye (NAMBA TATU) akimkabidhi Ilani ya uchaguzi  ya Chama cha mapinduzi mgombea huyo Namba tatu alisema kuwa kama Kembaki akifanikiwa na kuwa Mbunge ashugulikie ujenzi wa Soko ambalo olimebomolewa pamoja na kuleta maendeleo mengine kama vile  maji ambayo ni kero ndani ya Mji wa Tarime.

Wakati huo huo Katibu wa Chama cha mapinduzi wilaya Tarime,Khamis Mkaruka aliomba wanachama kuvunja makundi yaliyokuwepo wakati wa watia nia ili kuwaunga mkono wagombea wa Chama cha mapinduzi akiwemo mgombea Urais John Pombe Magufuli Wabunge na madiwani wote wa Chama cha mapinduzi na kuwapa kura zote za ndio.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *