Watuhumiwa wa Kuchoma Shule Wanaswa

October 19, 2020

 

Jeshi la Polisi wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro limefanyikiwa kukamatwa kwa watu watatu kwa tuhuma za kuchoma moto bweni la kulia chakula la wanafunzi wa Madrasa lililopo ndani ya Msikiti wilayani humo.

Bweni hilo liliungua kwa moto siku mbili zilizopita Ikiwa ni tukio la pili baada ya mabweni ya wanafunzi wa kike katika shule ya Kaloleni Islamic iliyopo Wilayani Moshi kuungua siku tatu zilizopita.

DC wa Hai, Lengai ole Sabaya na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo walifika eneo la tukio na kuvitaka vyombo vya dola kuweka nukta katika matukio hayo yanayoonekana ya kuratibiwa na kupangwa na kwamba katika wilaya hiyo litakua tukio la kwanza na la mwisho.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *