Watuhumiwa 32 washitakiwa kuwa wapiganaji wa kikundi cha uhalifu, on September 16, 2020 at 10:00 am

September 16, 2020

Watuhumiwa wengi wanakiri mashitaka dhidi yaoImage caption: Watuhumiwa wengi wanakiri mashitaka dhidi yaoKundi la watu 32 wako mahakamani nchini Rwanda kwa tuhuma za kuwa wapiganaji wa kundi la Rwanda National Congress RNC linaloendesha harakati zake mashariki mwa DRC.Baadhi yao wanaongozwa na meja mstaafu Wa jeshi la Rwanda,Habib Mudathiru ,wengine wakiwa askari watoro kutoka jeshi la Rwanda.Wanashitakiwa kujiunga na wapiganaji Wa kundi la RNC ambalo linaongozwa na Jenerali Kayumba Nyamwasa mkuu Wa zamani Wa majeshi ya Rwanda anayeishi uhamishoni nchini Afrika kusini.Kuna pia wengine waliojiunga na wapiganaji Wa vuguvugu la P5 ambalo pia linaendesha harakati zake mashariki mwa DRC.Wote walikamatwa katika mapigano mashariki mwa Congo mwaka 2019 na baadae kukabidhiwa Rwanda.Watuhumiwa wengi wanakiri mashitaka dhidi yao na kusema kwamba waliingizwa katika makundi hayo kwa nguvu. Kesi inaendelea.,

Watuhumiwa wengi wanakiri mashitaka dhidi yaoImage caption: Watuhumiwa wengi wanakiri mashitaka dhidi yao

Kundi la watu 32 wako mahakamani nchini Rwanda kwa tuhuma za kuwa wapiganaji wa kundi la Rwanda National Congress RNC linaloendesha harakati zake mashariki mwa DRC.

Baadhi yao wanaongozwa na meja mstaafu Wa jeshi la Rwanda,Habib Mudathiru ,wengine wakiwa askari watoro kutoka jeshi la Rwanda.

Wanashitakiwa kujiunga na wapiganaji Wa kundi la RNC ambalo linaongozwa na Jenerali Kayumba Nyamwasa mkuu Wa zamani Wa majeshi ya Rwanda anayeishi uhamishoni nchini Afrika kusini.

Kuna pia wengine waliojiunga na wapiganaji Wa vuguvugu la P5 ambalo pia linaendesha harakati zake mashariki mwa DRC.

Wote walikamatwa katika mapigano mashariki mwa Congo mwaka 2019 na baadae kukabidhiwa Rwanda.

Watuhumiwa wengi wanakiri mashitaka dhidi yao na kusema kwamba waliingizwa katika makundi hayo kwa nguvu. Kesi inaendelea.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *