Watu wenye ulemavu kurahisishiwa siku ya kupiga kura tarehe 28 Oktoba 2020,

October 1, 2020

Na Faruku Ngonyani , Mtwara

Kuelekea Uchaguzi Mkuu Tarehe 28 Oktoba 2020 ,Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa maelekezo kwa watendaji kutoa kipaumbele kwa makundi maalumu haswa kwa watu wenye ulemavu,Wajawazito,Wazee ,pamoja na Wagonjwa.

Hayo yamezungumzwa na Emmanuel Kawishe kwa niaba ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya ambae pia ni Mkurugenzi wa huduma za Sheria wa Tume alipokuwa anazungumza na wadau wa uchaguzi Mkoa wa Mtwara uliofanyika katika ukumbi Boma Mkoani humo.

Kuelekea Uchaguzi huo Tume ya Taifa ya Uchaguzi imefanya marekebisho ya kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2020 na kanuni za Uchaguzi wa Madiwani kwa mwaka 2020.

Aidha ameongeza kuwa kwa sasa Tume hiyo imefanya maandalizi ya Vifaa vya uchapishaji wa nyaraka mbalimbali zikiwemo fomu ,maelekezo kwa watendaji Uchaguzi  sambamba na kutoa maelekzo kwa vyama vya Siasa.

Lakini pia kawishe amewaasa wasiojua kusoma na kuandika kujitokeza siku ya kupiga kura kwa Tume imewaruhusu kwenda na mtu wanaowaamini kwa ajili ya kuwasaidia kupiga kura.

Kwa upande wa watu wenye ulemavu wa kutoona Tume ya Tifa ya Uchaguzi imeandaa kifaa cha maandishi ya nukta nundu (tactile ballot folder) aambapo itatumika kwa wale wanaoweza na kwa upande wa wasioweza kutimia kifaa hiko waenda vituoni na Mtu wanaomwamini ilim kusaidiwa juu ya upigaji kura.

 

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *