Watu wanne wameuwawa baada ya kuripuka kwa tanki la mafuta

October 11, 2020

Watu wanne wamefariki dunia baada ya kutokea mripuko katika tanki la mafuta katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut, na kuzisha hofu kwa wakazi wa mji huo kwa kurejesha kumbukumbu ya mripuko mwingine wa Agosti. 

Televishini ya Beirut imesema watu wengine 30 wamejeruhiwa, huku watoa tiba wakiongeza kusema watoto watatu wamelazwa hospitali kutokana na kupata majeraha ya kuungua. 

Kumetokea matuko ya moto kadhaa katika bandari ya Beirut, baada ya mkasa ya Agosti 4, ambao ulisababisha vifo vya watu 203, wengine takribani 6,500 kujeruhiwa baada ya athari zake kuvuruga makazi ya watu. 

Mripuko huo unatokea katika kipindi ambacho Lebanon inakabiliana na mdororo mbaya zaidi wa kiuchumi tangu 1975-1990 uliotkana na vita vya wenyew kwa wenyewe na mzozo wa kisiasa, hali ambayo imezongwa pia na janga la virusi vya corona.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *