Watu 90 wauawa katika mapigano mapya baina ya Serikali ya Syria na kundi la IS,

October 7, 2020

 

Mapigano kati ya vikosi vya serikali ya Syria na masalia ya wanamgambo wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS yameuwa watu wasiopungua tisini mwezi huu, hii ikiwa ni kwa mujibu wa shirika linalochunguza haki za binadamu nchini Syria, likiwa na makaazi nchini Uingereza. 

Shirika hilo limesema ndege za kijeshi za Urusi zimefanya mashambulizi ya kuwaunga mkono wanajeshi wa serikali ya Syria ambao ni washirika wao. 

Aidha, shirika hilo limeripoti kuwa mapigano makali yametokea katika maeneo mawili ya jangwani lililo kati ya bonde la Orontes na mto Euphrates. 

Kwa mujibu wa shirika hilo la kuchunguza haki za binadamu nchini Syria, wanajeshi 41 wa serikali wameuawa katika mapigano hayo, nayo IS imewapoteza wapiganaji 49. 

Mkuu wa shirika hilo Rami Abdulrahman amesema miongoni mwa hao, wanajeshi 10 wa serikali ya Syria na wanajihadi 13 wameuawa katika muda wa saa 24 zilizopita.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *