Watu 9 wafariki kwenye shambulizi la kujitoa mhanga nchini Afghanistan,

October 2, 2020

Watu 9 wameripotiwa kufariki kutokana na shambulizi la kujitoa mhanga liliotekelezwa kutumia la bomu lililolipuliwa kwenye kituo cha ulinzi wa usalama kilichopo Helmand nchini Afghanistan.

Msemaji kutoka ofisi ya mkuu wa wilaya ya Helmand, Omar Zuvak, aliarifu kwamba mshambuliaji huyo wa kujitoa mhanga alitumia gari lililotegwa bomu na kulenga kituo cha usalama mjini humo.

Miongoni mwa watu waliofariki kwenye shambulizi hilo ni maafisa 5 wa usalama pamoja na raia 4. Zuvak aliongezea kusema kuwa mtoto 1 pia aliweza kujeruhiwa.

Hadi sasa hakuna aliyedai kuhusika na shambulizi hilo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *