Watu 4 wafariki kwenye mlipuko wa ghala ya mafuta Lebanon,

October 11, 2020

Watu 4 wameripotiwa kupoteza maisha kwenye mlipuko uliotokea ndani ya ghala ya kuhifadhia mafuta iliyoko katika mji mkuu wa Beirut nchini Lebanon.

Mlipuko huo mkubwa ulisababishwa na moto uliozuka mida ya jioni, ndani ya ghala iliyohifadhiwa mafuta na raia mmoja  wa mtaa wa Tarik Jedide mjini Beirut.

Kikosi cha wazima moto kiliwasili katika eneo la tukio na kufanikiwa kuudhibiti moto huo ndani ya muda mchache.

Katibu Mkuu wa Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Lebanon George Kittana, alitoa maelezo kwa shirika rasmi la habari la taifa la NNA, na kubainisha kupatikana kwa miili ya watu 4 walipoteza maisha kwenye mlipuko huo.

Wizara ya Afya pia imetangaza kuwa itasimamia gharama za matibabu ya watu waliojeruhiwa kutokana na mlipuko huo.

Wakati huo huo, raia aliyehifadhi mafuta kwa ajili matumizi ya kampuni yake ya kibinafsi ameripotiwa kutiwa mbaroni baada ya tukio hilo.

Lebanon ambayo imekuwa ikikabiliwa na mzozo mkubwa wa kiuchumi katika historia, imekuwa ikikumbwa na uhaba wa mafuta kutokana na upunguwaji wa thamani ya sarafu  ya nchi. Hii imesababisha wananchi wa Lebanon kuanza kujihifadhia mafuta.

 

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *