Watu 100,000 wamekufa kwa COVID-19 nchini India,

October 3, 2020

 

India leo imefikisha idadi ya vifo 100,000 vilivyotokana na janga la virusi vya corona na kuwa taifa la tatu duniani kwa kiwango kikubwa cha vifo vya COVID-19 nyuma ya Marekani na Brazil.

Takwimu jumla zinaonesha kuwa wilaya za mjini ndiyo zimerikodi karibu asilimia 80 ya idadi ya watu waliokufa lakini wataalamu wameonya juu ya kuongeza kwa idadi ya vifo kwenye maeneo ya vijijini nchini humo. 

Maafisa wa afya wanasema marufuku isiyo na mpangilio ya kufunga shughuli za kawaida iliyolazimisha maelfu ya wafanyakazi kuondoa mijini na kwenda vijijini imezidisha ugumu wa kupambana na janga la virusi vya corona. 

Waziri Mkuu Narendra Modi na serikali yake ya chama cha kizalendo cha Kihindu wamekosolewa kwa jinsi wanavyoshughulikia kadhia ya corona na kuanguka kwa uchumi wa India kulikowaacha mamilioni ya watu bila ajira.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *