Watoto wa Rusesabagina wadai baba yao anaamriwa cha kuzungumza na mamlaka za Rwanda

October 2, 2020

Watoto wa Paul Rusesabagina na mwanasheria aliyeteuliwa na familia yake, wamesema kuwa ”ameamriwa na mamlaka za Rwanda” kitu gani cha kuzungumza na kuwa alikataliwa kuwa na wanasheria huru.

Bwana Rusesabagina ambaye alikuwa akitazamwa kama shujaa katika filamu ya Hollywood kuhusu mauaji ya kimbari nchini Rwanda, anashutumiwa kwa makosa 13 ya ugaidi.

Amekana mashtaka dhidi yake.

Katika mkutano na waandishi wa habari Alhamisi, watoto wake watano na mmoja wa mawakili saba walioteuliwa na familia yake kwa ajili yake, waliishutumu serikali ya Rwanda kwa kumnyima kupata “jopo lake la mawakili huru”.

Katika mahakama, Bw.Rusesabagina, 66, anasaidiwa na mawakili wawili kutoka muungano wa mawakili nchini Rwanda, ambao familia yake inasema kuwa ”walichaguliwa na serikali” na kufanya kazi kwa maslahi ya serikali.

Siku ya Ijumaa, mahakama mjini Kigali inajiandaa kutoa uamuzi kuhusu ombi la dhamana la Bwana Rusesabagina.

”Husema kilichoandaliwa”

Abana ba Paul Rusesabagina, umwunganizi washyizweho n’umuryango we n’umuvugizi w’ishyirahamwe rifasha yashinze mu kiganiro n’abanyamakuru kuwa kane tariki 01/10/2020

Peter Robinson wakili wa familia, alisema kuwa maelezo ya namna mbili yaliyotolewa na maafisa wa Rwanda kuhusu kukamatwa kwake yanathibitisha kuwa Bw Rusesabagina alitekwa nyara.

Mwezi mmoja uliopita wakati alifikishwa Kigali, wachunguzi wa Rwanda walisema alikamatwa na ushirikiano wa kimataifa.

Siku kadhaa baadaye Rais Paul Kagame aliiambia runinga ya serikali kwamba Rusesabagina alifikishwa Rwanda katika operesheni “isiyo na kasoro”

Katika mkutano na waandishi wa habari, Anaise Kanimba alisema bado hawajui ni vipi baba yake aliishia Rwanda.

“Na tunajua kwamba aliteswa ili kusema kile wanachotaka na walichiandaa” – aliongeza.

Akiwa chini ya ulinzi wa polisi, Bw Rusesabagina alinukuliwa na New York Times kwamba “alipanda ndege ya binafsi kwenda Bujumbura, Burundi” na kuishia Kigali

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *