Watoto wa Rusesabagina wadai baba yao anaamriwa cha kuzungumza na kuwa alikataliwa kuwa na wanasheria huru.

October 2, 2020

Dakika 12 zilizopita

Paul Rusesabagina yagaragaye mu rukiko yambaye umwenda w'abafungiye muri gereza zo mu Rwanda
Maelezo ya picha,

Paul Rusesabagina alizuiliwa nchini Rwanda

Watoto wa Paul Rusesabagina na mwanasheria aliyeteuliwa na familia yake, wamesema kuwa ”ameamriwa na mamlaka za Rwanda” kitu gani cha kuzungumza na kuwa alikataliwa kuwa na wanasheria huru.

Bwana Rusesabagina ambaye alikuwa akitazamwa kama shujaa katika filamu ya Hollywood kuhusu mauaji ya kimbari nchini Rwanda, anashutumiwa kwa makosa 13 ya ugaidi.

Amekana mashtaka dhidi yake.

Katika mkutano na waandishi wa habari Alhamisi, watoto wake watano na mmoja wa mawakili saba walioteuliwa na familia yake kwa ajili yake, waliishutumu serikali ya Rwanda kwa kumnyima kupata “jopo lake la mawakili huru”.

Katika mahakama, Bw.Rusesabagina, 66, anasaidiwa na mawakili wawili kutoka muungano wa mawakili nchini Rwanda, ambao familia yake inasema kuwa ”walichaguliwa na serikali” na kufanya kazi kwa maslahi ya serikali.

Siku ya Ijumaa, mahakama mjini Kigali inajiandaa kutoa uamuzi kuhusu ombi la dhamana la Bwana Rusesabagina.

”Husema kilichoandaliwa”

Abana ba Paul Rusesabagina, umwunganizi washyizweho n'umuryango we n'umuvugizi w'ishyirahamwe rifasha yashinze mu kiganiro n'abanyamakuru kuwa kane tariki 01/10/2020
Maelezo ya picha,

Watoto wa Paul Rusesabagina, wakili aliyeteuliwa na familia yake na msemaji wa shirika la kutoa msaada ambalo yeye ni mwanzilishi wake.

Peter Robinson wakili wa familia, alisema kuwa maelezo ya namna mbili yaliyotolewa na maafisa wa Rwanda kuhusu kukamatwa kwake yanathibitisha kuwa Bw Rusesabagina alitekwa nyara.

Mwezi mmoja uliopita wakati alifikishwa Kigali, wachunguzi wa Rwanda walisema alikamatwa na ushirikiano wa kimataifa.

Siku kadhaa baadaye Rais Paul Kagame aliiambia runinga ya serikali kwamba Rusesabagina alifikishwa Rwanda katika operesheni “isiyo na kasoro”

Katika mkutano na waandishi wa habari, Anaise Kanimba alisema bado hawajui ni vipi baba yake aliishia Rwanda.

“Na tunajua kwamba aliteswa ili kusema kile wanachotaka na walichiandaa” – aliongeza.

Akiwa chini ya ulinzi wa polisi, Bw Rusesabagina alinukuliwa na New York Times kwamba “alipanda ndege ya binafsi kwenda Bujumbura, Burundi” na kuishia Kigali.

Bwana Rusesabagina alikubali katika korti kuanzisha harakati za waasi za FLN, kikundi kilichoongoza mashambulio mabaya nchini Rwanda mnamo 2018 na 2019, lakini akasema haikuwa kwa sababu za ugaidi.

Bwana Robinson alisema kuwa Bw Rusesabagina aliye uhamishoni – ambaye ni raia wa Ubelgiji na mkazi wa Marekani – “hakuwa akiongoza shughuli za FLN”.

Watoto wake wamemuomba Rais wa Rwanda, ambaye msimamizi wa mkutano alisema kwa sasa yuko Marekani, amuachie baba yao mgonjwa, na kutoa wito kwa Ubelgiji na serikali ya Marekani kuingilia kati.

Rais Kagame alisema nini kuhusu kukamatwa kwa Bwana Rusesabagina?

Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema kwamba mpinzani wake mkuu Paul Rusesabagina alidanganywa akajileta mwenyewe nchini Rwanda.

Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu Rusesabagina kuoneshwa kwa vyombo vya habari ,Rais Kagame alisema kwamba lazima Rusesabagina awajibishwe kuhusu mauaji dhidi ya raia wa Rwanda kufuatia mashambulio ya makundi ya waasi anayoongoza yaliyofanywa dhidi ya maeneo ya Rwanda miaka miwili iliyopita.

Akizungumza kupitia runinga ya taifa,Rais Paul Kagame alisema kikubwa siyo ushujaa wa Bwana Rusesabagina au vitendo vyake wakati wa mauaji ya kimbari akisema kinachoangaliwa kwa sasa ni yeye.

kuwajibishwa kuhusu kwa vitendo alivyotaja kuwa vya mauaji dhidi ya raia wa Rwanda.

Katika matangazo ya moja kwa moja kwa televisheni ya taifa Bwana Kagame alisema kwamba hajali kuhusu hadithi ya Bwana Rusesabagina kwamba yeye ni shujaa wa mauaji ya kimbari na kwamba ”hilo si jambo ambalo litakalomkabili mahakamani”.

“Kuna maswali ambayo lazima atayajibu.kuna wanaomsaidia wakiwa Ulaya,Marekani na kwingineko na ambao walimpandisha cheo na kumpa majina ya ushujaa, awe shujaa au la ,mimi sina wasi wasi na hilo.

”Kikubwa tunachoangalia hapa ni kuhusika kwake na mauaji dhidi ya raia wa Rwanda, damu ya wananchi wa Rwanda iliyoko mikononi mwake kutokana na yeye kuongoza makundi ya kigaidi, lazima atawajibishwa kwa hayo” Alisema Rais Kagame.

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *