Watoto milioni 2 wanafia tumboni kila mwaka,

October 8, 2020

Mashirika ya kimataifa yamesema takriban watoto milioni 2 wanafia tumboni kila mwaka. Shirika la Afya Duniani, WHO, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia Watoto, UNICEF, pamoja na washirika wake wamesema vifo hivyo vinatokea zaidi kwenye nchi zinazoendelea. 

Kwa mujibu wa takwimu za dunia zilizochapishwa leo, mwaka uliopita vifo vitatu kati ya vinne vilitokea katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara au kusini mwa Asia. Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF, Henrietta Fore amesema kila sekunde 16, mama anapatwa na matatizo ya mtoto kufia tumboni. 

Ripoti hiyo imeonya kuwa janga la virusi vya corona linaloendelea, huenda likalizidisha tatizo hilo, ikikadiria kuwa kupungua kwa huduma za afya kwa asilimia 50 kunaweza kusababisha watoto zaidi 200,000 kufia tumboni mwaka ujao kwenye nchi 117 zinazoendelea. 

WHO imesema zaidi ya asilimia 40 ya watoto wanafia tumboni wakati wa kujifungua.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *