Watano wafariki dunia katika ajali iliyotokea Changombe Dar,

October 5, 2020

 

Watu watano wamefariki dunia huku wengine 10 wakijeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha basi dogo la abiria na lori la mchanga.

Ajali hiyo imetokea asubuhi ya leo katika eneo la mataa ya Chang’ombe, wilaya ya Temeke, Jijini Dar es salaam.

Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema waliokufa ni pamoja na wanaume watatu na wanawake wawili waliokufa papo hapo.

Kwa mujibu wa Kamanda Mambosasa, chanjo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi hilo kwa kushindwa kuzingatia taa za barabarani.

Kwa mujibu wa mashuhuda, ambao wengine walikuwa sehemu ya abiria kwenye basi hilo lililokuwa linatoka Temeke kwenye Muhimbili, wamesema pamoja na kumsisitiza dereva kuzingatia alama hizo, alipuuza kabla ya basi hilo kugongana na lori kwenye makutano.

Daktari Meshack Shimwela, Mganga Mkuu Hospitali ya Rifaa ya Temeke amesema kuwa wengine wanne waliokuwa katika hali zaidi walipata huduma ya kwanza na tayari wamepelekwa hospitali ya Muhimbili kwa tiba zaidi huku wengine waliojehuriwa wakiwa wanaweza kuendelea kupata matibabu katika hospitali ya Temeke.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *